Thursday 2 April 2015

HABARI ZAIDI TOKA KATIKA SHAMBULIO LA KIGAIDI KATIKA CHUO CHA GARRISSA KENYA.






Watu wenye silaha wameendesha shambulio Alhamisi asubuhi wiki hii katika Chuo kikuu cha Garissa, mashariki mwa Kenya, kilomita 150 kutoka kwenye mpaka wa Somalia.

Askari polisi wametumwa katika eneo la shambulio, ambapo milipuko inaendelea kusikika. Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, watu wawili wameuawa na wengine wanne wamejurihiwa.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, shambulio hilo lilianza saa za swala mapema asubuhi, kwenye majira ya saa kumi na moja na nusu leo Alhamisi. Idadi ya watu walioendesha shambulio hilo haijajulikana
Kwa mujibu wa gazeti la Kenya la The Standard, wanafunzi waliofaulu kuondoka chuoni hapo, wamesema waliwaona watu watano wenye silaha.
Kwa mujibu wa polisi ya Kenya, watu hao wenye silaha, walianza kufyatua risase walipoingia chuoni hapo. Walinzi wawili wameuawa. “ Mpaka sasa milio ya risasi imeendela kusikika katika Chuo kikuu cha Garissa, lakini ni vigumu kujua nani anayemrushia risasi mwengine”, mwakilisi wa polisi eneo hilo amesema, huku akibaini kwamba washambuliaji wamewateka nyara wanafunzi.
Wakati walinzi wa Chuo kikuu cha Garissa waliposikia milio ya kwanza ya risasi waliweza kujibu, lakini walizidiwa nguvu, na washambuliaji hao waliweza kufaulu kuingia katika chuo kikuu hicho.
Hata hivyo polisi na jeshi vimefaulu kuingia katika chuo kikuu Garissa, lakini mpaka sasa milio ya risasi na milipuko vimendelea kusikika.




Mwandishi wa habari wa Kenya Dennis Okari ambaye yuko katika eneo la chuo kikuu cha Garissa ameandika katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa:Wapiganaji hao wako katika jumba la kulala wanafunzi .''ninaweza kusikia milio ya risasi kutoka upande wa pili.@ntvkenya".


14.48pm:Mahitaji ya Damu:


kituo cha kutoa damu mjini Garissa

Kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ,Shirika la msalaba mwekundu Red Cross limewataka raia wa Garissa kutoa msaada wa damu.Walioitikia wito huo tayari wameeleka katika hospitali kuu ya Garissa mbapo kituo cha kutoa damu kilianzishwa chini ya mti.
14.40pm:Shahidi wa shambulizi:
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa Collins Wetangula amesema kuwa wakati wapiganaji hao walipoingia katika nyumba anayolala aliwasikia wakifungua milango na kuwauliza watu iwapo ni waislamu ama wakristo.''kama wewe ni mkristo unapigwa risasi papo hapo.kila mlio wa risasi nilipousikia nilidhani nitauawa'',aliambia shirika la habari la AP.Amesema kwamba maafisa wa usalama baadaye waliingia kupitia dirisha moja na kumtoa yeye na wenzake hadi katika eneo salama.
14.30pm:Maafisa wa matibabu kwa sasa wanaelekea katika hospitali ya kuu ya Garissa nchini Kenya ili kusaidia wale waliojeruhiwa
14.00pm:Kwa ufupi


Ramani ya chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya

Takriban watu 15 wanaodaiwa kufinika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Watu hao wanaodaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.


wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa

Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na wanafunzi wakijeruhiwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.
Mwandishi wetu anasema kuwa wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa.


Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho waliosalimika

Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.
13.40pm:Waislamu na wakristo waliotekwa ndani ya Jumba hilo la Chuo kikuu cha garissa wamedaiwa kutawanywa kabla ya waislamu 15 kuwachiliwa huru kulingana na msemaji wa kundi hilo la Alshabaab.
13.35pm:Serikali ya kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulihutubia taifa kufuatia shambulizi hilo la chuo kikuu cha Garrisa mapema leo.
13.30pm:Alshabaab:


Maafisa wa Polisi wa kenya

kundi la wapiganaji wa Alshabaab limesema kuwa liko ndani ya Chuo hicho kikuu na limewatawanya waislamu na wakristo
13.20pm:Wapiganaji wamedaiwa kuwateka nyara wanafunzi na kuwaua watu 14 katika chuo hicho kulingana na wafanyikazi wa msaada na maafisa wa polisi.Takriban watu 65 wengine wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia chuo hicho.Vituo vya habari nchini kenya hatahivyo vinaiweka idadi hiyo kuwa watu 16.
13.05pm:Idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi la wapiganaji wa kundi la alshabaab imefikia 14
13.03pm:Al shabaab


Alshabaab lakiri kutekeleza shambulizi

Kundi la wapiganaji wa Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa Kaskazini mashariki mwa Kenya huku likiwaua watu 14
12.47pm:Wanafunzi


wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya

Chuo hicho cha Garissa kina takriban wanafunzi 1000, na wafanyikazi wengine.
12.30pm Wanafunzi:


Wanafunzi waliodaiwa kutoroka

Baadhi ya wanafunzi wamedaiwa kutoroka kutoka mabweni waliokuwa wakilala
12.20pm:Wapiganaji


Wapiganaji

Wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa watano wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo la Chuo kikuu .
12.18pm:Kenya Red Cross


Maafisa wa polisi wakikabiliana na wapiganaji huko Garissa kenya

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema kuwa watu 30 wamejeruhiwa huku wanne kati yao wakiwa na majeraha mabaya..Kwa sasa shirika hilo linawasafirisha madaktari katika eneo hilo.
11.30am Idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya imefikia watu sita huku wengine 29 wakidaiwa kujeruhiwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!