Monday 6 April 2015

FURAHA YA SIKUKUU: Rais Kikwete awakumbuka watoto mahabusu Arusha

 Rais Jakaya Kikwete ametoa msaada wa mbuzi wawili, chakula na mafuta kwa watoto waliopo mahabusu mkoani hapa ili kusheherehea Sikukuu ya Pasaka.

Akikabidhi msaada huo, Ofisa Maendeleo ya Jamii Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha, Thabita Matiko alisema juzi kuwa vitu vyote hivyo vina thamani ya Sh400,000.
Alisema watoto hao wanapaswa kusherehekea Pasaka kama wengine wanaoishi na wazazi wao.
Wakati huohuo, Ofisa Ustawi wa Jamii, Mussa Mukamate aliiomba Serikali kujenga uzio katika mahabusu hiyo ili kuzuia watu wenye nia mbaya kuingiza dawa za kulevya.
Mukamate alisema pia wanahitaji wanasheria wa watoto hao ili kesi zao zilizoko mahakamani ziishe kwa muda mfupi, tofauti na hali ilivyo sasa.
Alisema kesi zinachelewa kutokana na kukosekana kwa wanasherisa wa kuwatetea watoto hao.
Pia aliliomba Jeshi la Polisi kuwa makini katika upelelezi wa kesi mbalimbali ikiwamo kuzingatia umri wa watoto ili kuepuka kuwapeleka wakubwa katika mahabusi hiyo.
“Tunaomba pia huduma ya usafiri, kuongezewa watumishi na matibabu ya dharura kwa mahabusi waliopo,” alisema.
Alisema kutokana na kesi hizo kuchukua muda mrefu, mahabusi hao wanakosa fursa ya kupata elimu na mbinu za stadi za maisha.
Mukamate alisema mahabusu hiyo inahitaji walimu wa kuwafundisha watoto hao wakati kesi zao zikisubiri kumalizika ili kuwapa ufahamu wa kuelewa mambo mbalimbali katika jamii.
Msimamizi wa mahabusu hiyo, Mussa Mapua alisema kuna mahabusi 17 kati yao 13 ni wa kike na wanne 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!