Sunday 22 March 2015

WAFANYABIASHARA WATESWA NA MGOGORO WA KENYA NA TANZANIA

 
Serikali imeombwa kuingilia kati mgogoro unaoendelea baina yake na nchi jirani ya Kenya, kuhusu kuzuiliwa kwa magari ya Tanzania ya kusafirisha watalii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata ili kuleta usawa na ustawi wa sekta ya utalii kwa nchi zote mbili.

Akizungumzia athari zinazotokana na mgogoro huo jana, mfanyabiashara maarufu nchini, Vicent Laswai akipanda Mlima Kilimanjaro alisema, Serikali imekuwa ikipoteza watalii wengi kutokana na magari yanayotoka nchini kutoruhusiwa kuingia katika uwanja huo wa ndege.
Alisema suala hilo linaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kupoteza mapato yanayotokana na utalii pamoja na kudidimiza sekta hiyo.
“Ingawa kunahitajika tafakuri ya kina kuhusu faida na hasara za mgogoro huo kwa Tanzania, kuna kila sababu Serikali yetu, ikaamka usingizini kwa kuwa wenzetu, wanaweza kutumia fursa hii kuendelea kujitanua na kuua ushindani wa kisekta… Ni vizuri ukatatuliwa haraka ili kutoa nafasi kwa wadau kuendelea na malengo ya kuvutia kimataifa,” alisema Laswai.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Marenga Investment, Joseph Kimoso alisema mgogoro huo, unahitaji ufumbuzi wa haraka.
Kisomo alisema ni vyema Watanzania waanze kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuliingizia taifa kipato, pamoja na mamlaka husika kuanzisha vilabu maalumu vya utalii.
Mkuu wa Idara ya Utalii ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), Eva Mallya akitoa taarifa yake, alisema mkakati endelevu wa Taifa unaolenga kuongeza idadi ya Watanzania kutembelea hifadhi nchini umeanza kuleta tija

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!