Thursday, 12 March 2015

MSAKO: WAGANGA WA KIENYEJI 55 WAKAMATWA MKOANI MWANZA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola (kushoto) akionyesha baadhi ya nyara walizokutwa nazo waganga hao.


Baadhi ya tunguli na nyara za serikali walizokutwa nazo waganga hao wasiokuwa na leseni.
Waganga hao pia walinaswa wakiwa na bendera ya taifa ambayo inadaiwa kutumiwa na wanasiasa pindi waendapo kwa waganga hao.
JUMLA ya waganga wa kienyeji 55 wasiokuwa na leseni wamekamatwa mkoani Mwanza katika oparesheni iliyofanyika kuanzia Machi 6, mwaka huu.
Akiongea na wanahabari leo jijini Mwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola amethibitisha kukamatwa kwa waganga hao 55 ambapo kati ya hao 18 ni wanawake na 55 wakiwa wanaume.
Oparesheni hiyo inayoongozwa na Kamanda Mlowola bado inaendelea ili kuhakikisha kuwa waganga wote wanaopiga ramli chonganishi wanakamatwa na kuhakikisha kuwa usalama wa maalbino unakuwepo na wanaishi kwa amani kama wananchi wengine.
Aidha Kamanda Mlowola ameongeza kuwa waganga hao wamekamatwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo ngozi za wanyama kama simba, kenge, ngozi za mijusi, ngozi za vinyonga vilivyokauka na vitu vinavyosadikika kuwa ni nywele za albino pamoja na meno ya albino lakini amesema kuhusu meno na nywele ataoa majibu sahihi baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanya vipimo juu ya vitu hivyo.
(PICHA ZOTE NA JOHNSON JAMES / GPL, MWANZA)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!