Friday 20 March 2015

MAREKANI IMESEMA BENJAMIN NETANYAHU AMEKIUKA MPANGO WA AMANI

Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu akifanya mashauriano na Raisi wa Marekani Bw. Barack Obama.


Msemaji wa serikali ya Marekani, Josh Earnest, amesema waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekiuka dhamira yake ya awali ya kuundwa kwa mataifa mawili kama suluhu ya mgogoro wa Israel na Palestina mwanzoni mwa wiki hii, na kwamba Marekani inautathmini msimamo wake upya.
Matamshi ya waziri mkuu huyo wa Israel ya kutotaka kuwepo kwa taifa la Palestina yanaonekana na wengi kama ndio yaliyomsaidia kushinda katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne.
Netanyahu amekiambia kituo cha televisheni cha Marekani, MSNBC, kwamba bado anabaki na dhamira ya kuundwa kwa taifa la Wapalestina, huku akikana taarifa za kubadili msimamo katika sera yake.
Bwana Netanyahu ameiambia MSNBC kwamba anataka Marekani na Israel kuendelea kuwa washirika wakubwa:
CHANZO: BBC SWAHIL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!