Tuesday 17 March 2015

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI MKONGE‏



Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkonge Ndugu Bahia Aboubakar wakati alipotembelea shule hiyo iliyoko katika Manispaa ya Lindi tarehe 17.3.2015.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkonge huko Lindi Manispaa wakashangilia kwa vigelegele wakati Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili shuleni hapo kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi na walimu tarehe 17.3.2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea risala ya Shule ya Sekondari Mkonge kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo Ndugu Bahia Aboubakar baada ya kuisoma.



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkonge bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha kwani wanafunzi hao walikataa kuahirisha mkutano wao na Mama Salma kutokana na shauku kubwa waliyokuwa nayo ya kuongea na mama huyo wa taifa.



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa Shule ya Sekondari Mkonge mara baada ya kutembelea shule hiyo tarehe 17.3.2015.





Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM Mama Sama Kikwete akipanda mti katika eneo la Shule ya Sekondari ya Mkonge mara baada ya kutembelea shule hiyo pamoja na kuongea na wanafunzi.

Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Salma Kikwete akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Tawi la Jamhuri lililoko katika Kata ya Jamhuri, Lindi Mjini kwenye mkutano wa ndani tarehe 17.3.2015.

PICHA NA JOHN  LUKUWI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!