Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam
Mayingu akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya inayoshughulikia
masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya walipotembelea Makao Makuu ya PSPF,
jijini Dar es salaam.Kushoto ni viongozi wa Kamati hiyo Mhe. Diana Chilolo,
Makamu Mwenyekiti na Lediana Mg’ong’o, Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Lediana Mg’ongo akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati kamati anayoiongoza ilipotembelea makao makuu ya mfuko huo leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. George Yambesi na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu.'
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Lediana Mg’ongo akiongoza kikao cha wajumbe wa
kamati yake na watendaji wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF, jijini Dar es salaam. Mhe. Lediana Mg’ong’o ameupongeza
uongozi wa mfuko huo kwa ubunifu na usimamizi mzuri wa mipango ya maendeleo
inayowanufaisha wanachama wa mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi Mfuko wa
Pensheni wa PSPF Bw. Bw. Abdul
Njaidi akiwapatia fomu za kujiunga na
Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na
Madawa ya Kulevya walipotembelea PSPF jijini Dar es salaam. Mtanzania yeyote
yupo huru kujiuga na mpango, akiwa katika sekta binafsi au sekta rasmi na haka
akiwa mwanachama wa Mfuko mwingine wa hifadhi ya Jamii.
Wajumbe wa Kamati ya ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mfuko wa Pensheni wa PSPF mara baada ya kuhitimisha ziara yao makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es salaam
Wajumbe wa Kamati ya ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mfuko wa Pensheni wa PSPF mara baada ya kuhitimisha ziara yao makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment