Mwanamitindo, mtangazaji muimbaji na muigizaji wa filamu, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, ametembelea kituo cha watoto yatima kilichopo maeneo ya Ubungo jijini Dar kisha kuangushiwa dua ya nguvu na watoto wa madrasa.
Wikiendi iliyopita Jokate alifika kituoni hapo kutoa misaada mbalimbali huku akiwa amejitanda kichwa chake ambapo alijumuika na watoto hao naye akakaa kwenye mkeka ndipo akazungukwa na watoto hao yatima kisha kuombewa dua ili abarikiwe na mambo yake yaende vizuri.
“Nilifurahi kuombewa dua na watoto. Hata hivyo, mimi sioni kama kuna tatizo, kikubwa zaidi Mungu tunayemuabudu ni mmoja ambaye anamsikiliza kila mtu kwa hiyo hakuna shida mimi kuombewa Kiislam,” alisema Jokate
1 comment:
aziz bilal23:32
Dua ni dua hakuna cha ajabu waja wa mwenyezi mungu inaruhusiwa kuombeana
Post a Comment