Ifuatayo ni hotuba yake ya kung'atuka ubunge na uanachama wa chadema aliyokusudia kuitoa 19/03/2015. Na clip ya video kimuonesha anavyoliaga bunge tarehe 20/03/2015
Mheshimiwa Spika, nilijiunga na Bunge lako tukufu mwaka 2005 nikiwa kijana mdogo mwenye malengo ya kupaza sauti ya vijana kwenye masuala yanayohusunchi yetu na pia kutetea maslahi ya wananchiwa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma.
Katika kudumu kwangu kama mbunge nililelewa na kukuzwana chamacha siasa cha CHADEMA ambacho kupitia chamahiki niliingia Bungeni. Chamahiki kilinilea na kunikuzatangu nikiwa na umri wa miaka16 na kupitia chamahiki nimejifunza mambo mengi sana. Nimeijua nchi yangu, nimejua siasa na nimejulikana ndani na nje ya nchi. Nitakuwa mwizi wa fadhilanisipotoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa CHADEMA na viongozi ambao nimefanyanao kazi muda wote nikiwa mwanachamana kiongozi.
Mheshimiwa Spika, Chamakilinikuza kama mwanasiasa lakini watu wa Kigoma Kaskazini ndio walionipa kiti hiki ninachokaliakama Mbunge. Juzi nilipokuwa nyumbani nilipata fursa ya kuwashukuru rasmi wananchikwa imani waliyonipa kuwatumikia kwa vipindi viwili mfululizo. Wengi wenu ndugu zangu wabunge mnafahamu,mihula miwili sio jambo la mchezo, sio lelemama. Mola atawalipa wananchiwa Kigoma kwa imani kubwa walioionyesha kwangu na kuniwezesha kulitumikia Taifa langukwa namna nilivyolitumikia.
Mheshimiwa Spika, nachukuafursa hii leo kuzungumziasuala la muda mrefu sasa la kutoelewana kati yangu na chamachanguna hivyo kuleta msuguano kati ya wananchi walionichagua kuwawakilisha na chamanilichopitia na kupeperusha bendera yake wakati wa uchaguzi mkuu. Licha ya msimamo wangu wa siku zote kwamba wananchipekee waliomchaguamwakilishi wao ndio wawe na mamlaka ya kumwondoa kwenye uwakilishi mchaguliwahuyo, mfumowetu wa kikatiba na mfumowetu wa kisiasa haupo hivyo na umeamua vinginevyo.
Mheshimiwa Spika, kwamba chamacha siasa kinaweza kumvua uanachamamwanachamawake na hivyo kupoteza kiti chake cha uwakilishi wa wananchiwake ni moja ya makosa makubwaya kikatiba ambayo tumeendelea kuyakumbatia, nimekuwa nikipinga na nitaendelea kupinga udikteta wa vyama dhidi ya utashi wa wananchi.
Mheshimiwa Spika, licha ya upinzani wangu mkali wa vifungukandamizi vya kikatiba, kama mzalendo ninaiheshimu Katiba yetu na mfumo wetu wa sasa na ninaheshimu uamuzi wa mahakamadhidi ya kesi yangu na sitakata rufaa. Hatua itakayofuatani uamuzi wa chamachanguna baadhi ya viongozi wameshatangazakwa umma kupitia vyombo vya habari kunivuauanachama ingawa sijapewa taarifarasmi.
Mheshimiwa Spika, ningeweza kukata rufaa kuhusumaamuziya mahakamakwani kunasababu lukuki ya kushinda rufaahiyo. Lakini ninadhani nimepigania haki zangu kwa muda mrefu sasa. Nimepigania kupanua wigo wa demokrasia ndani ya chamachangukwa muda mrefu sasa. Lakini ugomvi huu hauna manufaakwa pande zote husika, kwa hakikaunatuumizawote. Mimi ni mwanademokrasia. Naamini katika siasa za ushindani ndani ya chamana katika mfumomzima wa siasa kitaifa. Lakini sitakuwa tayari kudhoofisha harakatina kazi kubwa walizofanya wanamageuziwaliotutangulia kwa kuendeleza ugomvi unaotuumiza. Hivyo niko tayari kukubali kukaa pembeni. Ninaamini kuwa mapambano ya kuleta mabadiliko ya kweli na demokrasia katika nchi yetu Tanzania ni makubwakuliko mimi, kuliko kiongozi yoyote wa Chadema na kuliko wanachamawa Chadema.
Mapambano haya ya mabadiliko si kwa ajili ya kizazi hiki tu bali kwa vizazi vijavyo. Ndiyo maanasiku zote nimesema Nchi kwanza, vyama baadae. Kuona makundi yanajitokeza ndani ya harakatihizi, na kuwa na uhasama mkubwa uliopindukia, unawakatisha tamaa wananchiwanaotutumaini kuleta siasa iliyo tofauti na siasa za sasa. Muda umefika wa kupiga mstari na kuanzaupya. Hivyo nimeamuakuwa nitatii maamuziya chamaya kunivuauanachama na kung’atuka ubunge.
Mheshimiwa Spika, naomba niweke wazi kuwa nimefikia uamuzi huu kwa utashi wangu mwenyewe na nimepewa Barakazote na wananchi wangu na wazee wa Jimbo la Kigoma Kaskazini. Najua Watanzaniawengi ambao nimewatumikia kwa moyo wangu wote katika kipindi cha miaka hii 10 wanawezawasikubaliane na uamuzi huu. Hata hivyo Watanzaniawajue kuwa mfumowetu wa siasa na katiba unatoa nguvu kwa vyama vya siasa kudhibiti wabunge wake. Naamuahivi kwa sababu wenzangu ndani ya chamaambao nimehangaikanao usiku na mchana kujenga chamana kukifisha hapa kilipo hawapo tayari kufanyakazi tena na mimi. Nimesoma na kusikia kauli nyingi zinazoweka wazi kuwa hawanitaki ndani ya chama. Nimejitahidi kwa njia zangu zote kuona kama tunaweza kuendelea kufanyakazi pamoja ya kujenga mfumomadhubuti wa vyama vingi nchini lakini imekuwa ngumu kama mwanachamamwenzao. Ninaheshimu uamuzi wao huo.
Mheshimiwa Spika, kwa miakakumi hii si yote niliyafanyasahihi, yapo ambayo niliyakosea kama mwanadamukatika kufanyakazi kwangu, kwa namna yeyote ile naomba radhi Watanzaniawote kwa yote ambayo sikuyafanyakwa usahihi. Mimi ni binadamu, kiumbe dhaifu, sijakamilika. Ni Mola peke yake amekamilika.
Mheshimiwa Spika, siwezi kuanzamaisha yangu mapya bila ya kulishukuru Bunge lako tukufu, Bunge la Tisa chini ya Mzee Samwel Sitta na Bunge la Kumi chini yako Mama Anna Simamba Makinda. Bunge limekuwa ni nyumbani kwangu kwa takribani muongo mmoja. Nimekuzwa, nimejifunza, nimepambana, nimefurahina nimelia ndani ya Bunge hili. Kwa pamoja tumepigania maslahi ya wananchiwetu na kupingana na kufanyamambo kwa mazoea na hivyo kuleta mabadiliko kadhaa. Ni kipindi hiki ambapo wabunge tumekuwana sauti, Bunge la Tisa lilijenga ‘Bunge lenye Meno’ katika kupambana na ufisadi. Bunge la Kumi limejenga ‘Bunge lenye nguvu’ katika mfumowa Bajeti ya nchi yetu. Kupitia Bunge hili tumeweka misingi ya kujenga mfumomadhubuti wa uwajibikaji katika nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, wakati Bunge la Tisa litakumbukwa kwa hoja ya Buzwagi iliyopelekea nchi yetu kufanyamabadiliko makubwakatika mfumowa uendeshaji wa sekta ya madini (Sera mpya ya Madini na Sheria mpya ya Madini ) na hivyo mapato ya sekta ya madini kuongezeka kutoka Tshs 32 bilioni kwa mwaka mpaka Tshs 450 bilioni kwa mwaka hivi sasa; Bunge la Kumi litakumbukwa kwa hoja maalumu ya Tegeta Escrow iliyopelekea mfumowetu wa maadili ya Viongozi kupitia Barazala Maadili kuanzakufanya kazi kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa katika miakailiyopita. Mimi kuwa sehemu ya mabunge yaliyotekeleza hatuahizo za mabadiliko ni jambo la kujivunia sana.
Mheshimiwa Spika, kwa familia yangu, wajumbe wa PAC, tumekuwanguzo kubwa ya kujenga uwajibikaji wa Serikali kwa Bunge na wananchi. Napenda kuwashukuru kwa dhati kabisa kwa kuniungamkono na kwa kunipa ushirikiano kama Mwenyekiti wao. Changamotona malezi mliyonipa kwa miakayote hii yamejengaMtanzania mmoja mwenye dhati ya kuitumikia nchi yake, muda wowote, wakati wowote na kwa namna yeyote ile bila woga wala upendeleo. Nawashukurukwa kujitoa kwenu kwa nchi yetu na dhamira isiyo na mawaa ya kujenga Taifa imara zaidi.
Nitaendelea kuwatumikia wananchiwa Kigoma Kaskazini na Taifa languhata kama nimelazimika kuachia nafasi yangu ya ubunge kwa kipindi hiki kilichosalia kwa kusimamia ukweli, kutetea demokrasia ya kweli na kupigania maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida bila ubaguzi wowote.
Nitaendelea kuwatumikia wananchiwa Kigoma Kaskazini na Taifa languhata kama nimelazimika kuachia nafasi yangu ya ubunge kwa kipindi hiki kilichosalia kwa kusimamia ukweli, kutetea demokrasia ya kweli na kupigania maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida bila ubaguzi wowote.
Mheshimiwa Spika, Kwa CHADEMA, licha ya tofauti zetu ambazo zimekua kiwango cha kutosameheka, najivunia kwa fursa mliyonipa kuwa sehemu ya Barazahili la Taifa ambalo leo ninalihutubia kwa mara ya mwisho kama mbunge wa Kigoma Kaskazini. Fursa iliyonifanya niweze kuitumikia nchi yangu na mkoa wangu wa Kigoma. Inawezekanatusiweze kuelewana katika masuala ya uongozi, misingi na itikadi, lakini ninaamini tunapaswa kuelewana na kukubaliana katika kubwa ya kuijenganchi yetu kuwa Taifa linalojitegemea na lisilo na aina yeyote ya ubaguzi. Taifa lenye uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira na kuondoa umasikini, ujinga na maradhi, Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ni matumainiyangu kuwa tutakuwa bega kwa bega katika harakatihizi katika siku zijazo. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, nafasi hii ya kihistoria tuliyopewa haihitaji siasa za ubinafsi na unafsi!Uzalendo wetu utapimwa kwa uwezo wetu wa kuwekatofauti zetu binafsi pembeni kwa lengo lililo kubwa zaidi yetu.
Mheshimiwa Spika, Mwisho kwa wananchiwa Jimbo langu, wana Kigoma na raia wote wa Tanzania ambao kwa ridhaa yao nimekaakatika viti hivi kwa miakatakribani kumi, nawahakikishia kuwa dhamira yangu kuwatumikia, nia yangu na sababu za kutoa utumishi wangu kwenu vimekuwa na nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Huu ni mwanzo mpya. Ngugi aliandika ‘a grain of wheat’ kwa maanaya kwamba ‘Ili Mbegu iweze kumea lazima ife kwanza’.
Asanteni sana
CHANZO: SIMU .TV
No comments:
Post a Comment