Wednesday 18 March 2015

FAMILIA YA ALIYETEKWA WALIA NA POLISI WATEKAJI

Sintofahamu ya alipo muuguzi wa Mwananyamala, Pili Amiri imeendelea kuigubika familia ya muuguzi huyo na Jeshi la Polisi baada ya watekaji hao kushindwa kumuachia huru licha ya kupewa Sh5 milioni walichotaka.

Pili alitekwa Alhamisi ya wiki iliyopita maeneo ya Mwananyamala na watu wasiojulikana  ambao walitoa masharti ya kupewa kiasi hicho cha fedha ili wamwachie huru.
Fatuma Mbasa, shangazi yake Pili Amiri alisema , tangu watume kiasi cha Sh2 milioni za mwisho jana, hawajapata taarifa zozote za  kutia matumaini  kutoka kwa watekaji au polisi.
Alisema mara baada ya kutuma fedha hizo jana, watekaji walituma ujumbe  kupitia simu ya Pili wakiahidi kuwa atarudi jana asubuhi jambo ambalo halikufanyika.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema bado hawajapata taarifa zozote kuhusu kupotea kwa msichana huyo lakini aliahidi kuwa polisi inaendelea na uchunguzi.
Taarifa kutoka Hospitali ya Mwananyamala zinaeleza kuwa saa chache kabla ya kutekwa, Pili alionekana maeneo ya Mwananyamala akiwa amependeza.
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!