Msichana huyo inaonekana alitobolewa macho na watu wasiofahamika..
Mama ambaye anaishi jirani na eneo ambalo tukio hilo limetokea amesema kuwa walipata taarifa na kwenda eneo la tukio kuangalia, akakuta mwili wa binti ambaye anaonekana kuchomwa kisu shingoni na kutobolewa macho pamoja na kuingiliwa kimwili kabla ya kuuawa.
Mama huyo amesema tukio hilo linaonekana kutokea jana usiku kwa kuwa eneo hilo ni njia ambayo watu wengi wanaitumia.
Taarifa za tukio hilo zilifika Kituo cha Polisi na askari muda mfupi baadaye walifika eneo la tukio hilo.
VIA-MILLARDAYO.COM
No comments:
Post a Comment