Rahma Mashamu ambaye ni mama mzazi wa watoto wawili mmoja wa miaka 11 na mwingine 15 wanaodaiwa kubakwa na baba wa watoto hao akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na mwandishi wa habari.
Wakizungumza nyumbani kwao jana watoto hao, walisema baba yao alikuwa akiwatishia kuwakatakata kwa panga au kuwakaba koo humohumo chumbani endapo wangethubutu kumweleza mtu yeyote kitendo wanachokifanya.
“Tulikuwa tumeingia kwetu kulala na wadogo zangu, nikasikia
ananiita nikambembeleze mtoto eti anamsumbua, nilikwenda nikambembeleza akalala,
wakati nashuka kitandani kurudi
chumbani kwetu baba akanivuta kwake akanivua, akasema anachokifanya ni suna kwa
hiyo hataki kelele, akisikia atanikaba nife.”
“Niliumia sana na asubuhi mama alirudi nikajitahidi kweli
asijue na hata shule sikwenda, jioni mama aliondoka tena baba hakuniita siku
hiyo lakini baada ya siku tatu aliniita tena ikawa vilevile navumilia. Siku
zilivyozidi unaweza kukuta kwa wiki naitwa hata mara nne siku ambazo mama
hayupo nyumbani,” alisema.
Watoto hao walieleza kuwa baadaye baba huyo alihamia kwa
binti mdogo kwa staili ileile na kila mmoja alikuwa akiitwa kwa zamu na kwa vile
kila mmoja alijua ni siri yake na baba. Kutonaka na woga wa kuuawa, hakuna
aliyemweleza mwenzake hadi katikati ya mwaka jana mmoja wao alipomweleza
mwenzake na baadaye kumweleza mama yao.
“Baba alikuwa anasema atatuua bila hata mtu kujua na
tutaozea shambani, hata nikiwa katika siku zangu baba ananiingilia hivyohivyo,
naugua kila mara UTI, mdogo wangu naye kila mara UTI, tukaamua liwalo na liwe
kama kufa basi ila mama ajue,” alisema mtoto huyo huku akibubujikwa na machozi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miembe Saba, Hamis Shomari
alisema kabla ya kupelekwa kituo cha polisi Kongowe Jumamosi iliyopita, watoto
hao waliitwa shuleni hapo na kuhojiwa kila mmoja peke yake na wote walikiri
kuanza kubakwa mwaka 2013 na baba yao na kwamba tabia hiyo iliendelea hadi
Machi 19 usiku alipobakwa binti mdogo kwa mara ya mwisho na Machi 20 walipoamua
kumweleza mama yao.
Kamanda wa Polisi
mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema wanamshikilia mtuhumiwa huyo na kwamba
wasichana hao wamefanyiwa vipimo mbalimbali na majibu ya daktari yamethibitisha
kuwa wamebakwa na sehemu zao za siri
zimeharibiwa, hivyo wanaendelea na matibabu.
No comments:
Post a Comment