Tuesday, 24 March 2015

AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MANNE YAUA WATU WATANO-TABORA

Eneo la tukio,magari yakiwa yameharibika vibaya baada ya kutokea ajali katika eneo la Undomo wilayani Nzega mkoani Tabora usiku wa kuamkia leo-Picha zote na Sammy Poneka na Elizabeth Aloyce-Malunde1 blog Nzega



Gari aina lenye namba T654ACQ aina ya Pajero likiwa eneo la tukio
Gari aina lenye namba T654ACQ aina ya Pajero likiwa eneo la tukio
Basi lililohusika katika ajali

Sehemu ya basi
Gari aina ya Toyota Canter yenye namba T831ASK
Gari aina ya Toyota Canter yenye namba T831ASK

Eneo la Tukio
Eneo la tukio


Gari aina ya Landcruisera ikiwa imeharibika vibaya eneo la Undomo Nzega


Moja ya magari yaliyopata ajali

Miili ya watu watano waliokuwa kwenye landcruiser

Marehemu Yasinta Alex mmoja wa waliokuwa kwenye Landcruiser pamoja na maafisa wa TFDA na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega,ambaye enzi za uhai wake alikuwa na Duka la Dawa za binadamu pale Isunga Nzega-Picha zote na Sammy Poneka na Elizabeth Aloyce-Malunde1 blog Nzega

Watu watano wamefariki dunia papo hapo katika kijiji cha Undomo wilayania Nzega mkoani Tabora baada ya magari manne kugongana jana Jumatatu saa nne usiku


Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema haya:

"Ilikuwa ni gari ya halmashauri ya wilaya ya Nzega yenye namba SM 4905 ilikuwa na abiria watano,dereva na abiria wengine watatu ambao ni wafanya kazi wa TFDA walikuwa wanatokea Nzega Ndogo kwa ajili ya shughuli za mambo ya maduka",

"Walipofika eneo la Undomo gari hiyo ilikuwa inataka Kulipita gari jingine,ikaenda kugonga gari namba T654ACQ aina ya Pajero,kuna gari nyingine tena Toyota Canter yenye namba T831ASK,ikaenda mbele zaidi ikagonga basi la Super Kenny namba T874CWD likitoka Mbeya kwenda Mwanza".

"Watu watano waliokuwa kwenye Landcruiser ya halmashauri ya wilaya ya Nzega wamefariki dunia,akiwemo dereva aliyejulikana kwa jina la Charles Sanga na afisa utumishi wa halmashauri hiyo Peter Stephen",alieleza Kamanda Bwire.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa basi lililohusika katika ajali hiyo lilipasuka tairi la mbele lakini dereva wake alijitahidi sana na matokeo yake abiria wake kujeruhiwa tu na hakuna aliyepoteza maisha katika basi hilo.

"Gari iliyosababisha ajali hiyo ni hiyo Landcruiser iliyokuwa imeenda kufanya ukaguzi pale Nata,walipomaliza kufanya ukaguzi waakaanza kunywa bia mbili tatu,kisha kuanza safari kuelekea Nzega,lakini walipofika kona ya Undomo gari likapoteza mwelekeo,basi lilipandilia gari hilo dogo,watu wote ndani ya gari dogo wakafariki dunia papo hapo", shuhuda wa tukio hilo Furaha Titus ameieleza Malunde1 blog.

  KWA HISANI YA MALUNDE BLOG

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!