Sunday, 1 February 2015

WATU 96 RAIA WA BURUNDI WAKAMATWA KWA UJANGILI KATAVI

Jeshi la polisi nchini limefanikiwa kuwakamata watu 96 wengi wao wakiwa ni raia wa nchi jirani ya burundi, wanaotuhumiwa kujihusisha na ujangili kwenye hifadhi ya taifa ya katavi ikiwa ni pamoja na mapori mbalimbali ya akiba (game reserve) mkoani katavi, na kukutwa na silaha nne pamoja na risasi 118 na radio call kwa ajili ya mawasiliano.



Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi mrakibu mwandamizi wa polisi FOCUS MALENGO, akiongea mjini mpanda amesema mafanikio hayo yanatokana na operesheni maalumu iliyofanywa na askari wa jeshi hilo la polisi kutoka mikoa ya Dar na Tanga, kwa ushirikiano na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, ikiwa na lengo la kupambana na vitendo vya ujangili vinavyoendelea mkoani humo vinavyohatarisha uwepo wa baadhi ya wanyama na raslimali nyingine ambazo ni vivutio vya utalii.



Hata hivyo kaimu kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoani katavi hakuwa tayari kufafanua juu ya baadhi ya watuhumiwa hao ambao wamehamishwa kutoka mkoani katavi, mahali walikohamishiwa na idadi yao, ingawaje inaaminika kuwa ni raia wa nchi ya jirani ya burundi, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ujangili, na kuishi katikati ya mapori yaliyoko mkoani katavi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!