Friday, 6 February 2015

UGANDA YAILIPA TANZANIA FIDIA YA BIL 15.5

 

Serikali ya Tanzania imepokea takribani shillingi bilioni 15.5
 kutoka Serikali ya Uganda ikiwa ni fidia itokanayo na athari
 za vita vya Kagera.

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima ameeleza hayo
 Bunge mjini Dodoma kuwa fidia iliyokuwa inatakiwa 
kulipwa ni Dola za Marekani milioni 18.4 ingawa 
Uganda imelipa Dola milioni 9.7 zilizoingizwa 
kwenye mfuko mkuu wa Hazina.

“Kiasi hicho cha fedha kilipokelewa na kuwekwa
 katika Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ajili 
ya matumizi ya maendelao ya wananchi ”
 alisema Malima.

Alibainisha kuwa taratibu za fidia zitokanazo 
na hasara za vita hiyo zinaongozwa na 
sheria na kanuni za kimataifa pamoja na utaratibu
 wa kutathmini kiwango cha hasara kitokanacho na vita.

Aliongeza kuwa licha ya kwamba vita hivyo viliathiri
 taifa zima la Tanzania, mkoa wa Kagera umepokea
 fedha kutoka Mfuko Mkuu wa serikali ambayo imesaidia 
kusukuma maendelao ya wananchi.

Chanzo: wavuti.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!