JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/36 12 February 2015
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) anatarajia kuendesha usaili na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanyika kabla ya mtihani wa mchujo kuanza.
2. Kwa wale wasiokuwa na mtihani wa mchujo usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
7. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
8. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
9. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
2
10. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zinazohusiana na sifa zao zitakapotangazwa.
11. Kada zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo wazingatie mahali na tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa kwenye tangazo.
No comments:
Post a Comment