Ndege inayoimilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei na kuua watu 12.
Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema watu zaidi ya 50 walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakati ajali ilipotokea na idadi kubwa ya watu wameripotiwa kujeruhiwa.
Shirika la Habari la Taiwan limeonesha picha ya ndege hiyo ikiwa imezama kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung.
Chanzo cha ajali bado hakijajulikana.
Watu kadhaa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wengine 10 bado wamenasa katika ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan Taipei kuelekea uwanja wa ndege wa Kinmen nje ya Taiwan.
No comments:
Post a Comment