Wabibi (Shabani Ramadhani) ni msanii mkali na anayekuja kwa kasi katika soko la muziki wa Bongo Fleva hapa nchini Tanzania, Africa Mashariki na Dunia kiujumla.
Wabibi alizaliwa mwaka 1991 huko Tanga, akiwa anamiezi kadhaa wazazi wake walifariki wote ndipo alipochukuliwa na kwenda kuishi na shangazi yake, kwahiyo aliishi maisha ya upweke toka akiwa mdogo sana na kwa shangazi yake ndipo alipokulia mpaka alipomaliza elimu yake ya shule ya msingi.
Baada ya hapo Wabibi alianza maisha ya kujitafutia mwenyewe ili aweze kupata mahitaji yake ya kila siku katika kuhangaika kwa kipindi kirefu alijikuta akiuza maji ya chupa kama Machinga ndani ya Kituo cha Mabasi ya mkoa ya ubungo na huko ndipo alipata tumaini la kutimiza ndoto zake lilipo patikana, kutokana na ukarimu pamoja na uaminifu wake na kuongea na watu vizuri kulingana na umri wake alijikuta anapendwa na kila mtu ndipo alipokutana Mr. Wiliam Riwa ambaye alikuwa mteja wake wa maji wa kila siku. Sasa sikumoja William aliamua kujua historia fupi ya maisha yake ndipo alipogundua kwamba anakipaji cha kuimba na akaamua kumfadhili mpaka kufikia hapa na kuwa meneja wake.
Mwaka 2014 safari yake ya muziki ilianza kuonyesha mafanikio na kutoa nyimbo yake ya kwanza ya KITENGE aliye mshirikisha Mesen Selekta na kushoot na video yake pia ambapo video alifanya na Director Abbas Juma, na nyimbo ilipokelewa vizuri na mashabiki kutoka katika kila kona ya nchi mpaka kuweza kupata fursa ya kutumbuiza show za FIESTA na kupata interview za radio na television nyingi.
MSIKIE HAPA NA KIBAO KIPYA-NINENEPE
No comments:
Post a Comment