Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda anatarajiwa kufungua mkutano wa Nne wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF utakaofanyika tarehe 18 na 19 Februari 2015 katika Manispaa ya Dodoma.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni, ‘PSPF- chaguo lako sahihi’.
Taarifa iliyotolewa na Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF Bi. Costantina Martin, inasema mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ya wadau inayofanyika kila mwaka kwa lengo la kupata fursa ya kukutana na wadau wa Mfuko, kutoa taarifa ya mwaka ya Mfuko na kupokea maoni na ushauri kwa ajili ya maendeleo ya Mfuko.

Katika mkutano huo PSPF itapata fursa ya kutambulisha kwa wanachama na wadau Mkopo wa elimu na mkopo wa kuanza maisha, Bi. Martin alisema; “mikopo hii hutolewa kwa wanachama wa PSPF wakiwa bado kazini ili kutimiza malengo yao mbalimbali.
Meneja huyo alisema mafao mengine yanayotolewa na PSPF ni pamoja na; mafao ya uzeeni, malipo ulemavu, malipo ya mirathi, rambirambi ya mazishi, pensheni ya wategemezi, mafao ya kuachiswa kazi na fao la kujitoa.
Pia alisema pamoja na kutoa mikopo ya elimu na mkopo wa kuanza maisha, PSPF inatoa mikopo ya nyumba na mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu.
PSPF ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa na sheria ya Mafao ya Hitimisho la kazi kwa watumishi wa Umma namba 2 ya 1999 sura ya 371.
No comments:
Post a Comment