Majeshi ya Uganda yamekuwa yakimsaka LRA, Jamhuri ya Afrika ya Kati |
Jeshi la Uganda limesema limegundua mabaki ya kamanda
mwenye cheo kikubwa katika kundi la waasi la LRA.
Okot Odhiambo alikuwa mmoja wa makamanda watano
waliopatikana na hatia katika mahakama ya uhalifu wa kivita.
Inaaminiwa kuwa kaburi lake limegunduliwa katika
Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Msemaji wa jeshi la Uganda, Paddy Ankunda aliiambia BBC
kuwamajeshi ya Marekani yalikuwa yakifanya uchunguzi wa asidi
nasaba (DNA) kujua iwapo ni mabaki ya mwili wa Bw Odhiambo au la.
Kamanda mwengine wa LRA, Dominic Ongwen, alifikishwa mahakama
ya ICC wiki iliyopita.
Mkuu wa waasi hao, Joseph Kony, bado hajulikani alipo.
Mkuu wa waasi hao, Joseph Kony, bado hajulikani alipo.
No comments:
Post a Comment