Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimetangaza timu 18 zilizofanikiwa kutingia katika hatua ya 18 bora (raundi ya pili) ya michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam.
Timu hizo ni kutoka katika kundi (A) ambazo ni Red Coast,Yanga U20,Changanyikeni na Ukonga UTD,kundi (B) Simba U20,Stakishari,Zakhem na Beira Hotspurs,kundi (C) FFU,Sifa UTD,Pan Africa na Sinza Stars,huku kundi (D) likitoa timu za Shababi,New Kunduchi,Ugimbi na Azania Ngano.
Timu mbili zilizopata nafasi ya kuongezwa kwenye hatua hiyo ya pili,ni Sifa Politan FC pamoja na Tuamoyo FC,zinazokamilisha idadi ya timu 18.
Makatibu wakuu wa timu zote 18,wanatakiwa kufika katika ofisi za DRFA zilizopo kwenye jengo la Machinga Complex Ilala (Ghorofa ya 3),siku ya jumatano 04/02/2015,saa 8 mchana,kukutana na kamati ya mshindano kwaajili ya kupata utaratibu.
Baada ya kikao hicho DRFA itapanga makundi na kutoa ratiba ya kuanza kwa patashika hiyo.
No comments:
Post a Comment