Watuhumiwa wawili katika tukio la Ujambazi lililotokea Mchana wa leo eneo la Darajani Jua Kali,Zanzibar wametiwa mbaroni baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi wenye hasira wakati walipokuwa wakiwakimbia Polisi.
Watuhumiwa hao,ambao walikuwa na gari aina ya Toyota Noah lenye nambari za Usajili T 736 CGT na majina yao hayakufahamika mara moja,walijikuta wakipokea kipigo kikali kutoka kwa wananchi,baada ya gari lao hilo kushindwa kuendelea na safari baada ya kungia kwenye njia ambayo hairuhusiwi.
Askari Polisi pamoja na raia waliokuwepo eneo la tukio wakiwa wamemzunguka mmoja wa watuhumiwa hao wa ujambazi baada ya kumtia mbaroni mchana wa leo,katika eneo la darajani Jua Kali,Zanzibar.
mmoja wa watuhumiwa hao akiwa chini ya ulinzi ndani ya Gari la polisi.
No comments:
Post a Comment