MAHITAJI
3 Mayai
240 gram unga wa ngano ( Self raising flour)
120 gram castor sugar
1 Kijiko kikubwa cha chakula castor sugar
1 Kijiko kikubwa cha chakula maji ya vugu vugu
120 gram apricot jam, au trawberry jam au chocolate au custard
1 Kijiko kikubwa cha chakula icing sugar
Siagi kidogo iliyoyeyushwa kwajili ya kubrushia
JINSI YA KUANDAA
Pasha oven kwa moto 200º C. Paka siagi iliyoyeyushwa kwenye chombo utakachotumia kuokea keki yako (flat baking tray) Kisha weka karatasi isiyopitisha mafuta kama huna basi tumia karatasi nyeupe isiyo na mistari kumbuka nayo kuipaka siagi vizuri na uiweke katika chombo utakachotumia kuokea.
Chukua mayai pamoja na sukari tumia mashine ya kuchanganyia changaya mpaka mchanganyiko wako uwe laini na utoe mapovu kabisa.
Baada ya mchanganyiko huo kua laini safi na mapovu chukua unga na anza kuchanganya safi kwa kutumia kijiko fatilia picha hapo chini.
Kisha mimina mchanganyiko wako safi kabisa na usambaze vizuri uenee sehemu zote kwa usawa.
Choma kwa dakika 8 - 10 mpaka sponge iwe imeiva safi
Kisha chukua karatasi mpya isiyopitisha mafuta (baking paper) kisha ilaze juu ya meza safi. Nyunyiza juu ya baking paper kijiko kimoja cha castor sugar. Pole pole itoe cake yako kwenye chombo ulichookea na ihamishie kwenye baking paper mpya kisha nyunyiza tena castor sugar.
Hatua inayo fata ni kuweka mchanganyiko wa ladha yeyote ile unayopenda na ndio itakayo beba jina zima la chakula chako hichi mfano ukiweka jam itaitwa jam swiss roll na ukiweka chocolate itaitwa chocolate swiss roll au ukiweka custad itaitwa custad swiss roll.
Baada ya kuweka ladha ya chochote ukipendacho wewe hakikisha tendo hili unafanya haraka haraka kabla cake yako haijapoa itakua vigumu kuikunja, anza na pindo dogo dogo mpka uikunje yote iwe duara kwa kuzungusha na kumbuka karatasi lazima ibaki nje. Acha na karatasi mpaka ipoe ndani ya freezer ili ishikane kabisa ikisha poa kabisa a kushikana toa karatasi.
Unaweza nyunyizia kwa juu icing sugar. Kwakutumia kisu kikali kata slice saafi kabisa tayari kwa mlaji kufaidi.
Chukua mayai na sukari weka kwenye bakuli
Tumia machine ya mkono kwa kuchanyania mpaka iwe safi na laini
Mayai na sukari vimeanza kuchanganyika vizuri na rangi ya kiini cha yai inabadilika toka kwenye njano kali na kua njano iliyofifia
Hapa rangi inazidi kufifia na mchanganyiko unachanganyika safi kabisa
Hapa imechanganyika bado kidogo tu itakua tayari
Sasahapa ipo safi na imekua laini na imeweka mapovu imeshapanda na kuongezeka
Weka unga ndani ya mayai haya na unaze kuchanganya pole pole
Changanya kwakutumia kijiko cha chuma au mwiko wa mbao poe pole ili mayai yenye sukari na unga viweze kuchanganyika safi bila kuweka mabonge bonge
Pole pole endelea kuchanganya
Mpaka mchanganyiko wako sasa unakua laini na umechanganyika safi kisha mimina kwenye chombo cha kuokea na choma kwa dakika 8 - 10 kisha toa
Hapa imeiva safi na inaonekana na rangi nzuri ya kahawia itoe haraka kabla haijapoa na weka kwenye karatasi mpya ya kuokea ukiwa umesha nyunyiza sukari yako nyeupe ya chenga
Sasa hapa ipo safi unaweza kuweka mchanganyiko wa ladha yeyote uipendayo na uanze kukunja
Kama nilivyoelekeza awali kua kunja kwa kuanzia kunjo dogo mpaka unamaliza mduara wote hakikisha karatasi inabaki nje kama picha hii inavyoonyesha ili swiss roll yako ikamilike
Kumbuka usikunje kama picha hii inavyoonyesha karatasi ikabaki ndani ule mchanganyiko wako wa ladha ulioweka ndani utashikana na karatasi na hautaweza kuitoa ukiitoa inamana utakua umesha ikunjua swiss roll yako na haitaweza kurudi katika umbo lake tena na utakua umepoteza maana halisi. Na mlaji itabidi ale na karatasi hahahaaaaaaaaaa!
Ukifata maelekezo vizuri swiss roll yako baada ya kupoa vizuri kwenye freezer na ukatoa karatasi ya juu itakua na muonekano huu na hiii ni swiss roll yenye mchanganyiko wa srawberry na custard.
Tumia kisu kikali kata slice safi wapatie familia wafurahie baada ya chakula au chai ya jioni saa 10
Hii ni swiss roll ya ladha ya machungwa na mchanganyiko wa karanga kati kati.
Huu ni muonekano wa chocolate swiss roll
SIO NGUMU KUTENGENEZA NI UFATILIAJI MZURI TU WA JINSI YA KUANDAA HAICHUKUA MUDA MREFU KUANZIA KUANDAA MPAKA KUPIKA NA KUIVA NI DAKIKA 45 TU IFURAHISHE FAMILIA YAKO KWA UBUNIFU.
ENJOY
No comments:
Post a Comment