Thursday, 29 January 2015

WAARABU WAGOMA KUMSALIMIA MICHELLE OBAMA KISA HAKUVAA USHUNGI!


Rais Obama na Mkewe Michelle Obama, wamefupisha ziara yao walipokwenda kutoa heshima zao katika familia ya kifalme kwa kifo cha Mfalme Abdullah wa Soudi arabia kwani Michelle Obama hakuwa na furaha pale walipofanya ziara ya kwenda kuutana na mfalme mpya wa saudi arabia mfalme Salman.


habari zinasema kuwa Michelle Obama hakuonekana kuwa na furaha kutokana na jinsi wanawake wanavyonyanyaswa na mfumo dume lakini pia mapokezi aliyoyapata yeye hayakumfurahisha.

Inchi ya Soudi arabia ni nchi ambayo wanawake hawaruhusiwi kutoka au kutembea hadharani bila kuvaa ushungi, pia wanawake katika nchi hiyo hawaruhusiwi kuendesha gari yaani ni marufuku kabisa kwa mwanamke kuonekana anaendesha gari lakini pia wanawake hawaruhusiwi kabisa kuwa na akaunti benki na mambo mengine mengi


Lakini pia Mrs Obama hakufurahishwa na mapokezi, kwani waliposhuka kutoka ndani ya ndege walikutana na msafara wamapokezi ulioongoza na viongozi wa Nchi hiyo, lakini ajabu katika msafara huo ambao ni wanaume watupu, wengi wao walikuwa wakigoma kusalimia kwa kumshika mkono.
habari zinasema kuwa wengi wa waliokuwa katika msafara huo wakusalimiana na Rais Obama walikuwa wakikwepesha mikono pale walipotaka kusalimiana na Michelle Obama na badala yake kuishia kuinamisha vichwa tu.

Michele hakufurahishwa na kitendo hicho kwani pamoja na kujitahidi kuvaa nguo ndefu iliyofunika miguu yake lakini alionekana kama kavunja sheria ya nchi yao kwa kutokifunika kichwa chake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!