Wanasayansi wanaofuatilia ugonjwa wa Ebola nchini Guinea wamesema kuwa virusi vya Ebola vimebadilika tangu kubainika mgonjwa wa kwanza mwezi marchi mwakajana.
Watafiti kutoka taasisi ya Pasteur mjini Paris ambao wamekuwa wakichunguza sampuli mbalimbali za damu ili kuweza kutafuta namna ya kukabiliana na virusi hivyo wamesema virusi hivyo vinajibadili.
Kwa sasa wataalam hao wanachunguza pia kama mabadiliko hayo ya virusi yanaweza kubadili mfumo wa maambukizi ya ugonjwa huo.
Ugonjwa Ebola umewaua watu Zaidi ya 8000 huko Afrika Magharibi.
No comments:
Post a Comment