Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Josephine Kulea kutoka Taasisi ya Samburu Girls ya nchini Kenya mara baada ya binti huyo kutoa ushuhuda wake kuhusu namna alivyoathirika na ndoa za utotoni wakati wa mkutano wa Marais na Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika kuhusu kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni uliofanyika huko Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 29.1.2015. Binti huyo alijifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama Ban Soon Taek wakati wa mkutano wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika uliozungumzia kampeni ya kupiga vita ndoa za utotoni barani Afrika wakati wa kikao cha 24 cha Umoja huo kilichofanyika Addis Ababa tarehe 29.1.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Chad na Mwenyekiti wa Umoja wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (OAFLA) Mama Hinda Deby Itno wakati wa kikao kilichoandaliwa na Jumuia ya Afrika kuzungumzia kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani humo tarehe 29.1.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Niger Mama Malika Issoufou Mahamadou mara baada ya kuhudhuria kikao cha Umoja wa Afrika kuhusu kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani humo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Malawi Mama Gertrude Maseko Mutharika(wa kwanza kulia) pamoja na Mama Ban Soon Taek, Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (katikati) wakati wa kikao cha Wakuu wa nchi za AU kinachofanyika mjini Addis Ababa tarehe 29.1.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Margaret Kenyatta mara baada ya kuhudhuria kikao cha Umoja wa Afrika kilichozungumzia kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika mara baada ya kikao cha kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani Afrika. Wengine katika picha ni (kutoka kushoto kwenda kulia), Mama Ban Soon Taek, Mke wa Katiubu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mama Widad Babker, Mke wa Rais wa Sudan, Mama Salma Kikwete, Mama Hinda Deby Itno. Mke wa Rais wa Chad (mwenye begi mkononi), Mama Esther Lungu, Mke wa Rais wa Zambia, Mama Hadidja Aboubaker, Mke wa Rais wa Comoro, Mama Roman Tesfaye, Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mama MalikaIssoufou, Mke wa Rais wa Niger, Mama Margret Kenyetta na Mwisho ni Mama Gertrude Mutharika, Mke wa Rais wa Malawi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani Afrika. Wengine katika picha ni Mama Widad Babker ,Mke wa Rais nwa Sudan, Mama Esther Lungu, Mke wa Rais wa Zambia na Mama Margaret Kenyatta.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment