Wednesday, 21 January 2015

MSAADA! WADAU PIGA SIMU HII 0768 14 0069 KUTOA MSAADA KWA BINTI HUYU

Estha Sako akiwa na mwanaye

Pichani ni Mkazi wa kijiji cha Masagala wilayani Kishapu Estha Sako mwenye ulemavu wa ngozi(Albino) anayesumbuliwa na kidonda kikubwa usoni,ugonjwa ambao umemsumbua kwa muda mrefu.Hivi sasa anaishi maisha ya kuomba omba katika Senta ya Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga pia ana mtoto wake mwenye ulemavu wa ngozi ambaye hajaanza kusoma hivyo anahitaji msaada wa kupatiwa elimu.

Estha Sako ametekelezwa na mme wake,akiwa amezaa naye watoto wawili mmoja mwenye ulemavu wa ngozi na mwingine asiye na ulemavu wa ngozi.

Estha Sakoa anahitaji  msaada wa matibabu na kusomesha mtoto wake
Kama umeguswa na matatizo ya Estha Sako piga simu namba 0768 14 0069

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!