Bibi mwenye ulemavu wa viungo
 Sicholastica Mhagama (77), mkazi wa Kijiji
 cha Lundusi, 
Kata ya Maposeni, wilayani Songea, Mkoa 
wa Ruvuma, aliyeamua kujitengenezea jeneza lake
 kutokana na kuchoshwa na madhila ya dunia hii,
 hatimaye ameanza kupata misaada ya hali 
na mali kutoka kwa wasamaria wema mbalimbali.


Kwa miaka mingi, bibi huyo amekuwa
 akikabiliwa na matatizo kibao, hali
 iliyomlazimu, mwaka 1985,
 kujitengenezea jeneza na kufanya siri
 kubwa isipokuwa mmtu wake mmoja
 tu wa karibu
 aliyekuwa akifahamu siri hiyo.
Kaburi 1
Bibi Scholastica Mhagama (77) ambaye 
alijitengenezea jeneza hili mwaka 1985 
baada ya kutelekezwa na ndugu na jamaa zake
Mwandishi wa FikraPevu, kwa msaada
 wa mtu wake huyo wa karibu na bibi huyo, 
ambaye  jina lake linahifadhiwa kwa sasa ndiye
 aliyefanikisha mazungumzo bibi huyo
 kabla ya kutoboa siri hiyo ya kujitengenezea 
jeneza alilolihifadhi ndani ya nyumba yake
 kwa miaka takriban 30 sasa bila watu kufahamu.
Jeneza hilo, katika kulihifadhi, alilifunika
 na vitu
 vingine kiasi kwamba mtu hawezi kuliona 
hadi bibi
 mwenyewe aamue kuonyesha mahali lilipo. 
Mwandishi wetu alilazimika kuomba msaada
 wa watu
 wawili zaidi ili kuweza kulifukua kaburi hilo
kuliondoa ndani ya nyumba hiyo na kulibeba kwa lengo
 la kulitoa nje ili kuweza kupata picha nzuri likiwa
 nje ya nyumba ya bibi huyo.
“Nimetengeneza kabisa jeneza langu ili siku nikifa wanizike katika jeneza hili. Nimetengwa na jamii.
 Majirani wanashindwa kunisaidia kwa madai eti mimi ni mchawi…naumia sana kusingiziwa kitu
 ambacho sikijui,” anaanza kusimulia kwa masikitiko bibi huyo.
Kwa mujibu wa Bibi Mhagama, uamuzi huo wa kujitengenezea kabisa jeneza, ulitokana na imani
 kwamba pindi atakapokufa, hataweza kupata msaada wa maziko yenye heshima kwa kuwa jamii
 inayomzunguka, imeshindwa kumsaidia akiwa hai, hivyo anaamini kwamba siku atakapofariki dunia
 anaweza kutupwa tu kama mzoga.
Akisimulia baadhi ya mateso anayokumbana nayo kila siku, Bibi Mhagama anasema ni pamoja
 na ukosefu wa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, hali inayomlazimu kuoga mara moja kwa 
mwezi; kukosa huduma muhimu za malazi na chakula, akisema kwa miaka kadhaa sasa hajapata
 kula kitoweo cha nyama wala samaki.
Baadhi ya misaada ya haraka ambayo bibi huyo alikuwa anahitaji, ni pamoja na baiskeli ya miguu
 mitatu (wheel chair) ambayo itamwezesha kutembea kwa kuwa kwa sasa anapotaka kwenda
 mahali, hulazimika kutambaa chini hali anayosema inamsababishia maumivu makali kutokana
 na nyama iliyobakia kwenye nyonga baada ya kukatwa mguu wake tangu akiwa motto wa darasa
 la tatu.
Bibi 2
Bibi akipokea godoro, blanketi pamoja
 na vyakula baada ya kupokea msaada 
kutoka kwa 
Kelvin Nicholous wa Arusha
Kutokana na kilio hicho cha muda mrefu cha bibi
 huyo, hatimaye msamaria mwema mmoja
 anayeishi Marekani, baada ya kusoma makala 
inayomhusu bibi huyo mtandaoni ameguswa
 na kuamua kumpatia baiskeli ya miguu mitatu 
inayokadiriwa kugharimu zaidi ya Sh milioni moja
 pamoja fedha taslimu kiasi cha Sh 30,000 kwa ajili
 ya matumizi yake ya nyumbani.
Mwakilishi wa Msamaria huyo nchini hapa, 
Sephoroza Katanga, mwenye makazi yake jijini
 Dar es Salaam, mara baada ya baiskeli hiyo kuwasili
 bandari ya Dar es Salaam Septemba 
mwaka jana, aliwasiliana na mwandishi wa makala
 haya kwa ajili ya kujua utaratibu wa kuisafirisha
 baiskeli hiyo hadi Songea kwa ajili ya kumkabidhi
 bibi huyo.
Baiskeli ya Bibi copy
Baiskeli kwa ajili ya bibi Scholastica ambaye ni mwenye ulemavu, ambayo imeletwa
 na watu waliomtapeli kwa kumletea baiskeli feki
Hata hivyo, kwa kuwa Septemba hiyo mwaka jana
 mwandishi wa makala haya alikuwa 
masomoni akiendelea na kozi yake ya kimataifa 
kuhusiana na mafuta na gesi kwa ufadhili 
wa taasisi ya Revenue Watch Institute ya Marekani,
 ikijumuisha wanafunzi waandishi 
takriban 30 kutoka nchi za Uganda, Ghana na
 Tanzania yenyewe, hivyo alishindwa kushiriki 
katika hafla ya kupokea baiskeli hiyo, hali
 iliyomlazimu mwakilishi huyo kutafuta namna
 nyingine ya kufikisha baiskeli hiyo kwa mlengwa.
Kutokana na kukosa fursa hiyo Septemba 
mwaka jana, hivi karibuni Mwandishi wa
 makala 
haya alifika katika kijiji cha Lundusi, nyumbani
 kwa bibi Sicholastica ambapo ameonyeshwa
 baiskeli yenye magurudumu manne madogo 
ambayo anasema alikabidhiwa na watu wawili, 
Oktoba, mwaka jana, ambayo hata hivyo
 anasema tangu akabidhiwe, hajaweza kuitumia 
kutokana na muundo wa aina ya baiskeli yenyewe.
“Nimeletewa baiskeli hii yenye magurudumu madogo manne, lakini baadhi ya vifaa vyake ni vibovu.
 Tatizo jingine ni kwamba baiskeli hii ni ndefu sana
nashindwa kuipanda kwa hiyo tangu imefika, sijaweza 
kuitumia kwa kuwa siwezi hata kuiendesha…
inahitaji mtu wa kunipandisha na kunisukuma 
na mimi hapa naishi pekee yangu. Nadhani baiskeli ya magurudumu makubwa na ninayoweza
 kuendesha mwenyewe bila msaada wa mtu mwingine
, ingenifaa zaidi,” anasema Bibi huyo na kuongeza:  
 “Watu hao walifika hapa waliacha baiskeli na
 kuondoka. Siwajui hata majina yao, kwa kweli 
nahitaji ya baiskeli ya magurudumu makubwa 
ndiyo  inayoweza kumaliza tatizo langu kwa kuwa
 bado natambaa na kujivuta chini  siwezi kutumia 
baiskeli hii.”
Pamoja na Mwakilishi wa Msamaria huyo 
anayeishi Marekani anasema baiskeli aliyoipokea
 na kuikabidhi kwa watu waliyoileta hapa
 ilikuwa mpya yenye magurudumu makubwa, huku 
ikiwa na vifaa vya kisasa vya kumwezesha 
kuendesha yeye mwenyewe bila matatizo,
 lakini inayoonekana hapa inaonekana kama
 kuu kuu, tena magurumu yake yakiwa vipara
 hali inayotia shaka kwamba watu hao 
waliokabidhiwa kuileta, wanaweza kuwa 
waliichakachua
 kwa sababu bibi huyu anasema hata hizo
 Sh 30,000, ambazo Mwakilishi huyo anasema
 alizikabidhi pia, nazo hazikumfikia.
Bibi msaada tena (1)
Hapa ndipo mahali alipokuwa analala akiwa 
ameweka mfuko chini ambao ndiyo
 ulikuwa
 kitanda chake kwa miaka mingi
“Kijana mmoja kati yao niliowakabidhi 
wheelchair na fedha zile, ninamfahamu.
 Alijitambulisha
 kwangu kwamba ni waandishi. 
Nitafuatilia ili kuhakikisha vitu halisi ambavyo
 alitakiwa kupewa
 bibi huyo vinamfikia. Nimemwandikia
 baruapepe tayari Mfadhili kumfahamisha
 kuhusu utapeli 
huo na ameahidi kutuma baiskeli nyingine,” 
anasema Mwakilishi huyo.
Tatizo jingine kubwa ambalo lilikuwa 
linamkabili Bi Scholastica, ni ukosefu wa kitanda
 na godoro hali iliyomlazimu kulala 
chini kwa miaka yote kwa kutumia 
mifuko ya mbolea
 na kujifunika blanketi chakavu.
Msamaria mwingine mkazi wa jijini Arusha ambaye amejitambulisha kwa jina la Kelvin Nicholous,
 ametoa msaada wa fedha kwa Bibi huyo 
ambazo zimewezesha kununulia godoro, blanketi 
pamoja na mahitaji muhimu, ikiwemo sabuni,
 sukari, mafuta na matumizi mengine.
Kwa mujibu wa Kelvin, makala iliyotoka
 mtandaoni ikiwa imeandikwa na mwandishi
 wa makala
 haya kuhusiana na kisa hicho cha bibi huyo,
 cha kuamua kujitengenezea jeneza baada
 ya kuchoshwa na dhiki za hapa duniani,
 ilimgusa sana ndiyo maana angalau
 nimetoa msaada
 huu ili kupunguza baadhi ya matatizo 
yanayomkabili bibi huyo mwenye 
ulemavu wa viungo.
“Huo ni mwanzo tu, kwa sasa najipanga
 pia nitawashirikisha wenzangu kuhakikisha
 changamoto nyingine kama ya kibanda 
chake cha nyasi, kinaezekwa kwa bati ili bibi
 huyo asiendelee kuvujiwa hasa katika kipindi
 hiki cha masika,” anasema Kelvin.
Wachungaji wawili wa Kanisa la TAG 
Songea ambao hawakupenda majina yao kuandikwa
 ni miongoni mwa watu walioguswa na tatizo
 la Bibi Scholastica, baada ya kufika 
nyumbani kwake 
na kumkabidhi msaada wa Sh 60,000 ambazo 
anasema sehemu yake amezitumia kulimia
 shamba lake la mazao mbalimbali.
“Kuna Wachungaji wawili walifikishwa 
hapa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lundusi na
 kunipa msaada wa fedha taslimu kiasi 
cha Sh 60,000, kwa kweli nawashukuru sana,”
 alisema bibi huyo.
Bibi Scholastica ambaye ana uwezo mkubwa 
wa kujieleza, amekiri pia kupata misaada
 mingine
 midogo ya vyakula, mavazi na vitu vingine
 kwa ajili ya matumizi yake, kama vile sabuni na sukari
 kutoka kwa watu mbalimbali wa ndani 
na nje ya kijiji chake, ingawa anasema
 bado anahitaji
 msaada zaidi, hasa wa nyumba kwa 
kuwa nyumba anayoishi sasa licha ya kuvuja, lakini si
 salama kwake na mali zake.
“Miaka yote hii nimekuwa nalala chini. 
Godoro langu lilikuwa ni mifuko ya mbolea, 
lakini kwa sasa
 nimeletewa godoro na blanketi na ninapata
 usingizi mzuri…nawaombea wote
 walionisaidia Mungu
 awabariki sana,” anasema bibi huyo.

Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 pamoja na Sera ya Taifa ya Huduma na Maendeleo
 kwa Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2004
, zinaelezea kuhusu haki ya makundi hayo kupata
 matunzo katika jamii.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, 

inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 
2050, idadi ya wazee
 wenye umri wa zaidi ya miaka 60
 itakuwa itakuwa milioni 8.3, sawa na 
asilimia 10 ya idadi ya
 Watanzania wote.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 

1999, inaonyesha kuwepo kwa ongezeko 
la idadi ya wazee
 duniani, huku ikielezwa kwamba 
ongezeko hilo katika nchi zinazoendelea,
 halilingani na uwezo
 wa rasilimali zilizopo za kuwahudumia
 wazee katika nyanja za afya, lishe na huduma
 nyingine
 za msingi katika maisha ya binadamu.