Wednesday, 21 January 2015

JIZOWEZE KULA SALAD!



Wengi wetu si wapenzi sana wa kula salad, kiukweli ni kwamba salad ikitengenezwa kama ilivyo hainaga test kabisaa! kama mie nalia shida tu,kwa sababu ni lazima nile lakini wala sio chakula ninachokizimia NO!
Ni hivi kama salad ikitengenezwa vizuri na dressing, huleta radha tofauti,huwa ni nzuri na unaweza kula pekee bila chochote pembeni. Chungulia humu mpango mzima!

Mahitaji


Tango 1/2
Kitunguu 1/2
Cherry tomato 8
Lettice kiasi
Green olives kidogo
Black olives kidogo
Hoho jekundu 1
Carrot
Giligilani kidogo

Salad dressing
Yogurt 1/2 kikombe
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai
Chumvi kidogo
Olive oil kiasi

Matayarisho
Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa  katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.

Aina za salad unaweza kuchanganya na kitu chochote kwenye salad yako Angalia mfano hapo wa salad mbalimbali..




No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!