Friday, 23 January 2015

HATUHITAJI MSAADA WA UN-NIGERIA

Nigeria haihitaji msaada wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa kupambana na Boko Haram.Mshauri wa maswala ya usalama wa taifa nchini humo ameiambia BBC.


Sambo Dasuki amesema Nigeria na majirani zake Niger,Chad na Cameroon wanamudu kusshughulikia swala la Wanamgambo wa kiislamu.
Dasuki amekiri kuwa Wanamgambo ni tishio kubwa la usalama nchini humo na kusema kuwa takriban asilimia 50 ya Jeshi la Nigeria limepelekwa kaskazini mashariki .
Amesema hatua hiyo inaashiria namna Jeshi lilivyolichukulia swala hili kwa umakini mkubwa.
Alipoulizwa na Kipindi cha Newsday cha BBC kama Nigeria inahitaji msaada wowote wa nje , alisema ''hapana''
Wanamgambo wa Boko Haram walianza Operesheni yao mwaka 2009, wakidai kuwa wanataka kuunda taifa la kiislamu.
Tangu Serikali ilipotangaza hali ya hatari miezi 20 iliyopita kaskazini mashariki ili kupambana na Wanamgambo, kundi hilo limejiimarisha na sasa linadhibiti miji kadhaa .
BBC.

1 comment:

Anonymous said...

aziz bilal16:33


1


Wale wa west african kweli hawahitaji msaada toka UN kutatua shida yao na Boko Haram,wenyewe wanajitosheleza vya kutosha wana umoja wao unatosha sana kuifanya hiyo kazi.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!