Monday, 19 January 2015

Ghana kwa Senegal, Algeria v Bafana



Bata, Equatorial Guinea. Ghana itakuwa ikisaka kuendeleza ubabe wake dhidi ya Senegal wakati Algeria wataonyeshana kazi na Afrika Kusini leo katika wa kwanza wa Kundi C.

Senegal na Ghana zimekutana mara tatu kwenye mashindano ya Afrika na Black Stars ikishinda mara mbili na kutoka sare moja.
Black Stars wataingia katika mchezo huo wakiwategemea nyota wake Asamoah Gyan, Andre Ayew na Emmanuel Agyemang-Badu kuwaongoza katika mchezo huo mgumu dhidi ya Simba wa Teranga waliozaliwa upya.
Lakini, Ghana watakiwa kubadilika zaidi, baada ya kushindwa kuonyesha kiwango cha juu katika michezo ya kufuzu japokuwa walimaliza wakiwa vinara wa kundi.
Kocha mpya Ghana, Avram Grant aliyeichukua jukumu hilo wiki sita zilizopita atajaribu kutumia mfumo mpya pamoja na ule wa 3-5-2.
Hata hivyo, Senegal inayofundishwa na kocha Alain Giresse watakuwa wakimtegemea mshambuliaji wake Sadio Mane anayecheza Southampton kuongoza mashambulizi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!