Kyle Jones (31) akiwa na mpenzi wake, Karen, anasema huvutiwa tu na wanawake wanaomzidi umri kwa makumi kadhaa ya miaka.
Kyle akiwa kakolea katika hisia kali na mpenzi wake mzee zaidi aitwaye Marjorie McCool, mwenye umri wa miaka 91.
KYLE JONES wa Pittsburgh, Pennysylvania, nchini Marekani, aliye na umri wa miaka 31, ameelezea kuvutiwa kwake na wanawake ambao wanamzidi umri kwa makumi kadhaa ya miaka. Kijana huyo ameweka wazi kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, hajafanya mawasiliano yoyote ya kimapenzi na mwanamke aliye chini ya umri wa miaka 60.
Kyle ambaye alifichua hayo jana kipindi maalum cha kituo cha televisheni cha TLC kiitwacho ‘My Strange Addiction’ (Tamaa Yangu ya Ajabu), alisema mpenzi wake mzee zaidi wa kike ana umri wa miaka 91.
“Nawapenda wazee wa kike kwa kila kitu. Napenda harufu yao, napenda kuwa karibu nao na hisia zao,” alisema katika kipindi hicho kijana huyo ambaye alipokuwa na umri wa miaka 18 alikuwa tayari amepata mpenzi wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 50.
Kyle alianza kuvutiwa na wanawake wazee akingali shuleni ambapo mtu wa kwanza kumvutia alikuwa ni mwalimu wake aliyekuwa na umri wa miaka 65 wakati huo.
“Nilimpenda kwa nywele zake nyeupe, umbo lake, na kila kitu,” anasema.
No comments:
Post a Comment