Picha hii ni moja ya vingozi wa kundi hilo ambao kamishna kova aliwahi kuudhibitishia mtandao huu kuwa wamefanikiwa kuukamata mtandao wa wahuni hao lakini sasa wameibuka tena jijini Dar es salaam
Hali ya sintofahamu imetanda katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam usiku huu baada ya vijana wanaofanya fujo maarufu kama PANYA ROAD kuingia barabarani usiku huu kufanya fujo na kuvuruga hali ya amani katika maeneo kadhaa ya jiji la Dar es salaam.vijana hao wameanzia fujo hizo katika maeneo ya magomeni kagera na kusambaa maeneo yote ya magomeni,mabibo na kuelekea maeneo ya sinza na kufanya shughuli zote za kiuchumi kufungwa ikiwa ni pamoja na maduka na shughuli za ushafiri kusimama kwa muda kupisha vijana hao ambao haieleweki wanadai nini ila wao wanapiga kila wanayekutana naye mtaani.
Mwandishi wa mtandao huu ameshughuia maeneo ya sinza muda huu kukiwa hakuna shughuli zinazoendelea na badala yake wananchi wanalazimika kukaa majumbani mwao kuokoa maisha yao juu ya vijana hao ambao wanatembea kimakundi wakiwa na silaha a jadi kama mapanga,mawe na siaha nyingine.
Baadhi ya wanachi waliozungumza na mtandao huu wamelitupia lawama jesho la polisi kwa kushindwa kuwadhibiti vijana hao kwani wameanza hatakati hizi zamani lakini jeshi la polisi limekuawa likishindwa kuwachukulia hatua madhubuti kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa hawakai kwa amanai kuogopa fujo hizo.
Wananchi wanaoishi maeneo ya sinza,kwa mtogole,magomeni,mabibo na viunga vyake wanashauriwa kutokuzurura ovyo mitaani muda huu kwani vijana hao wapo maeneo hayo na bado hawajaondoka.
1 comment:
aziz bilalYesterday 23:47
1
Reply
Lumpen proletarians hawa wakiachiwa wanaweza wakageuka kuwa kundi baya sana ,history inatufundisha kuhusu vijana wa namna hii ktk nchi yeyote ile,nchi ya Algeria inaweza kuwa kigezo kizuri sana kuwaelewa vijana wa namna hii.
Post a Comment