Monday, 19 January 2015

150 WAPEWA MIMBA NA WANAFUNZI WENZAO CHUONI



Wanafunzi 150 kati ya 1,000 waliojiunga na masomo 

katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce)
 mwaka jana wamebainika kuwa na ujauzito waliopewa
 na wenzao chuoni hapo.



Utafiti wa usawa na jinsia uliofanywa na chuo hicho
 kati ya Juni na Novemba mwaka jana umebaini kuwa 
wanafunzi wanaopata ujauzito ni wale wa mwaka wa kwanza.

Hayo yamebainishwa jana na Mratibu wa Masuala ya Jinsia
 wa chuo hicho, Dk Dativa Shilla katika warsha ya uchaguzi
 na uhusiano wa kijinsia iliyofanyika chuoni hapo.

Alisema hali hiyo inatokana na kuwapo kwa vitendo vya ukatili, manyanyaso na ubabe unaofanywa na wanachuo wa kiume dhidi ya wale
 wa kike na hivyo kuwalazimisha kufanya mapenzi bila 
hiyari yao.

“Kupitia utafiti huu tumeona hakuna usawa wa kijinsia 
wa kupata elimu baina ya mwanamke na mwanamume 
kwa sababu mwenye ujauzito hawezi kufanya vizuri 
katika masomo yake ukilinganisha na mhusika wa kiume,” 
alisema.


Awali, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo cha Kumbukumbu 
ya Mwalimu Nyerere, Amon Katunzi alisema ni wakati sasa
 kwa Serikali kutoa mikopo kwa wanafunzi wote kwa sababu
 hatua hiyo itapunguza wanafunzi wa kike kujiingiza 
katika uhusiano wa kimapenzi kwa sababu watakuwa
 na fedha za kujikimu.

“Lengo la warsha hii ni kutoa elimu na ushauri kwa wanafunzi
 wa jinsi zote ili waweze kusoma vizuri na kuacha ushawishi
 wa kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi. Pia, tunawashauri 
hata wale ambao wapo katika ndoa wavumilie na kuepuka 
kupata ujauzito ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao,” alisema Katunzi.

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho Gosbeth 
Kihanga ambaye alikiri kuwapo kwa vishawishi chuoni
 hapo na kudai kuwa inachangiwa na ugumu wa maisha
 hasa kwa wanafunzi wa kike.

Alisema kupitia kongamano hilo wamejifunza na kuelewa
 mengi hususani katika suala la kupanga na kugawana
 majukumu, kubadilisha mtazamo na kuacha kutumia ubabe
 katika uhusiano wa mapenzi.

Chanzo: mwananchi.co.tz

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!