Wednesday 10 December 2014

VYOMBO VYA SHERIA VICHUKUE MKONDO WAKE HII TABIA YA KUWAVUA NGUO WANAWAKE NI UNYAMA NA UNYANYASAJI WA HALI YA JUU


Hii imetokea leo maeneo ya Buguruni Jijini Dar es Salaam



Vitendo vya wanawake kuvuliwa nguo mitaani vimekithiri, huu ni uonevu wa hali ya juu, kwanini wanawake tunanyanyaswa hivyo kiasi cha kukosa amani,Hii sasa ni "too much" Imekuwa ndio mchezo sasa, hii inaonyesha jinsi gani watu hawajaelimika, hawa wanaofanya vitendo hivi kwa kweli lazima serikali iwachukulie hatua, Tanzania ni nchi huru, msitake kutunyanyasa, hii sio Dubai ama uarabuni huko! mtu anauhuru wa kuvaa nguo anayotaka wewe kama unamapungufu yako tafuta msaada usaidiwe, Hii mimi naita ni unyanyasaji tena wa hali ya juu, chonde chonde vyombo vya dola kamata hawa wapuuzi wanaotudharirisha.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!