Maambukizi ya virusi vya Ukimwi yameshuka kwa asilimia 38 tangu mwaka 2001 na idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi vimepungua kutoka zaidi ya milioni 2.3 mwaka 2005 hadi milioni 1.5 mwaka 2013.Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani, Desemba Mosi ya kila mwaka, takwimu zinaonyesha juhudi zilizofanyika katika kupambana na ugonjwa huo.
Haya yakiwa maendeleo mazuri, bado idadi kubwa ya watu wapatao milioni 35 wanaishi na virusi vya Ukimwi. Kila siku zaidi ya watu 5,700 wanaambukizwa virusi vya Ukimwi, sawa na watu karibu 240 kila saa.
Ifikapo mwaka 2015, watoto milioni 25 watapoteza mzazi mmoja au wote wawili kutokana na ugonjwa wa UKIMWI.
Ugonjwa huu ni janga kubwa la kijamii duniani.UKIWMI si tu unawanyang'anya mamilioni ya watoto maskini kabisa, upendo na ulinzi kutoka kwa wazazi wao, bali pia watoto wengiwanabakia kuhangaika peke yao, wengi wakiwa na jukumu la kuwalea wadogo zao, katika hali ya umaskini mkubwa, kubaguliwa na unyanyapaa unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya HIV. Watoto wengi wanatengwa na mara nyingi ndugu wa familia zao hawawezi kuwatunza.
No comments:
Post a Comment