Saturday 6 December 2014

UPANDIKIZAJI WA MIFUKO YA UZAZI KWA WANAWAKE WENYE UGUMBA

Ugumba ni  la kifamilia linaloweza kusababisha manyanyaso kwa wanawake wengi katika ndoa. Tatizo hili pia linaweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa na hata wakati mwingine mwanamume kuoa mwanamke mwingine au kupata nyumba ndogo ili apate kuzaa.

Ugumba pia ni moja ya sababu za ongezeko la wizi wa watoto hasa katika vituo vya afya nchini.
Kwa wanandoa wanaopendana kwa dhati, hali ya kutokupata watoto inaweza kuwaumiza kisaikolojia na kuathiri vibaya hali bora ya maisha na furaha ya wanandoa hao.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ugumba kwa mwanamke ni hali ya kushindwa kupata ujauzito kama inavyotarajiwa baada ya miaka miwili ya kushiriki tendo la ndoa vizuri bila kutumia kinga au njia za kuzuia kupata mimba.
Tatizo la wanawake kushindwa kuzaa limegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni utasa na ugumba. Utasa ni ile hali ya kuwa na historia ya kutopata ujauzito kutokana na kuwapo kwa matatizo ya kimaumbile ya kuzaliwanayo yanayosababisha mwanamke asiweze kutunga mimba. Moja ya matatizo haya ni kuzaliwa bila kuwa na mfuko wa kizazi.
Takwimu za afya ya jamii, zinaonesha kuwa tatizo hili humpata msichana mmoja kati ya wasichana 4,500.
Sehemu ya pili ya tatizo hili ni ugumba, hapa mwanamke anakuwa tayari huko nyuma alishawahi kupata ujauzito, haijalishi alizaa au mimba iliharibika, lakini kwa sasa hana uwezo wa kubeba ujauzito bila kupata huduma maalumu za kitabibu.
Sababu za ugumba zinaweza kuwa ni kuondolewa kizazi kwa njia ya upasuaji kutokana na sababu kama vile saratani, mabonge, magonjwa katika mfumo wa uzazi au kuharibika kwa mirija ya uzazi.
Utafiti uliofanywa na Larsen na kuchapishwa mwaka 2000 katika jarida la kimataifa la epidemiolojia (International journal of Epidemioloy) toleo la 29, ulibaini kuwa tatizo la ugumba ni kubwa Tanzania ikilinganishwa na nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Zambia.
Akizungumzia ukubwa wa tatizo la ugumba, mmiliki wa Kituo cha utungishaji mimba kwa njia ya upandikizaji wa mbegu cha Nairobi (Nairobi IVF Centre), kinachohudumia Watanzania pia, Dk Joshua Noreh anasema:
“Tatizo la ugumba kwa sasa ni wastani wa asilimia 10, hiyo ina maana kwamba kati ya wanandoa 10 mmojawapo hana uwezo wa kushika mimba. “Kiwango hiki kwa sasa kinakua kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wanawake wa sasa kuchelewa kuolewa wakitoa kipaumbele kumalizia masomo.”
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili, Dk Henry Mwakyoma ambaye aliwahi kufanya utafiti kuhusu ugumba na kubaini kuwa asilimia 80 ya wanaume nchini wana tatizo la ugumba, anasema kuwa mfumo wa maisha wa sasa ndicho chanzo cha ongezeko la tatizo la uzazi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!