Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amethibitisha kutokea kifo hicho na kuongeza kuwa mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar
Aisha madinda ambae jina lake halisi ni Aisha Mbegu alizaliwa mwaka 1980 katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar na alipata umaarufu mkuwa kwa uhodari wake wakucheza muziki alipokuwa kwenye Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Vile vile Aisha aliwahi kuingia kwenye tasinia hii ya filamu na kuweza kuigiza filamu akiwana watu kama aliekuwa muimbaji TX Moshi William (Marehemu) pamoja na mcheza soka Boniphace Pawasa.
Taarifa zaidi juu ya msiba huu tutaendelea kukujuza kadri tuzipatapo.
Pole ziende kwa ndugu na jamaa na wote walioguswa na msiba huu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahari pema pemoni AMEN.
CRD: BONGOMOVIE
CRD: BONGOMOVIE
No comments:
Post a Comment