Tuesday, 9 December 2014

TANZANIA YAPOKEA MABEHEWA 22 YA ABIRIA NA 50 YA MIZIGO


Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia kitu wakati wa kupokea sehemu ya mabehewa ya kisasa yatakayotumika kuboresha usafiri katika reli ya kati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).kushoto ni Afisa Habari wa TRL,Midraji Mahezi.

Sehemu ya ndani ya Mabehewa hayo.
Serikali imepokea mabehewa 50 ya mizigo na mabehewa 22 ya kisasa ya abiria ikiwa ni sehemu ya mabehewa 274 yanayotawarajiwa kuwasili nchini ili kuboresha huduma za usafiri wa mizigo na abiria.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amesema kuingia kwa mabehewa hayo ni ishara ya jitihada za serikali katika kuimarisha huduma ya usafiri wa reli ambapo amesema serikali imetumia zaidi ya bilioni 200 katika kuboresha sekta ya reli nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la reli nchini, Kipalo Kisamfu amesema mabehewa hayo ya abiria ni kwa ajili ya safari katika mikoa ya Mwanza na Kigoma, na kusisitiza shirika hilo kwa kushirikiana na wakala wa usafiri wa majini na nchi kavu wako katika mchakato wa kuanzisha usafiri wa haraka wa abiria ambao utasimama katika vituo vikubwa pekee.
Picha: Ernest Nyambo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!