Friday 12 December 2014
MFUKO WA PENSHENI PSPF WATENGA BILIONI KWA AJILI YA MKOPO WA ELIMU
Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana
na Benki ya Posta Tanzania wamezindua huduma mpya kwa watejawake, huduma hizo ni Mkopo wa kuazia Maisha na Mkopo wa elimu.
Kwa upande wa mkopo wa elimu mwanachama anaweza kukopa
kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yoyote ile ya elimu,
mfano stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata
mafunzo ya ufundi. Katika huduma hii PSPF imetenga jumla
ya shilingi bilioni 4.Pia zipo Billioni 2 kwa kukopesha waajiriwa wapya
Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, mwanachama
aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa ana mahitaji muhimu,
kwa kutambua hilo PSPF imeanzisha mpango huu ambapo
mwanachama anaweza kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili
aweze kujipanga na maisha mapya ya ajira. Katika huduma hii
PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.
Lengo kubwa la PSPF kuanzisha mikopo hii ni kuhakikisha kila
mtanzania anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika masomo kwa
kupitia mkopo wa elimu au ndoto yake nyingine kwa kupitia
mkopo wa kuanzia maisha, hivyo natoa wito kwa watanzania
wenzetu kujiunga na PSPF ili waweze kufaidika na fursa hizi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Kazi na Ajira
Mheshimiwa Gaudentia kabaka alisema amefurahishwa na PSPF
jinsi ilivyoshirikiana na Benki ya Posta Tanzania katika Kubuni,
Kupanga, kuandaa na hatimaye kuteleza utratibu huu, alisema
hili ni jambo sahihi na mwafaka kwani kwa mujibu wa taratibu
za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii duniani kote, kazi za Mifuko hii sio
kutoa mikopo bali ni kuwawezesha wanachama wake kupata
mafao yao stahili pale wanastaafu.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,
Bw. Sabasaba Moshingi alisema mwanachama wa PSPF
anayetaka kukopa anatakiwa kwenda kwenye tawi lolote la Benki
ya Posta lililopo karibu yake. Huduma za utoaji wa mikopo hii ni
za haraka sana na bora.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment