Tuesday, 9 December 2014

KLABU ZA UKIMWI ZAOMBA KUUNGWA MKONO



SERIKALI imetakiwa kuvisaidia vikundi mbalimbali vinavyojitolea katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU), ili viweze kutoa elimu katika jamii dhidi ya ugonjwa huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Klabu ya Ukimwi ya Chuo Kikuu Huria Kanda ya Temeke, David Malangalila, alisema bila ya serikali kuongeza ushirikiano na vikundi hivyo, jamii itakosa uelewa na kasi ya ugonjwa huo itaongezeka.
Alisema kutokana na kasi ndogo iliyopo wilayani Temeke ya kupambana na ugonjwa huo, wakiwa kama serikali ya wanafunzi wameamua kufungua tawi la kwanza la kupambana na Ukimwi wilayani humo, lengo likiwa kuongeza kasi ya mapambano.
Kwa upande wake, Daktari wa Kitengo cha Ukimwi Hospitali ya Temeke, Dk. Luoga Andrew, alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuanzisha vikundi vya aina hiyo, kwani vinasaidia kutoa mchango wa elimu katika jamii.
Alisema kwa sasa mapambano ya ugonjwa huo nchini yanaridhisha na muelekeo wake ni mzuri, kutokana na watu kuhamasika kujitolea na kujitokeza kuanzisha vikundi ambavyo vinaibua changamoto mpya katika Wizara mbalimbali ikiwemo ya Afya.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!