Safari ya kuingia kwenye pori hilo kwenda kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo. |
Wakazi wa Mji wa Pongwe wakiuangalia mji huo kwa masikitiko makubwa. |
Huzuni ilitawala eneo hilo.
MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 27 mpaka 30 ambaye jina lake halijafahamika mpaka sasa amekutwa akining'inia juu ya mti wa Mwembe uliopo katika pori lililopo nje kidogo ya mji wa Pongwe, Mkoani Tanga.
Hali ya sintofahamu iliendelea kutanda katika eneo hilo huku kila aliyeweza kufika katika eneo hilo la tukio akiwa na mshangao wa kipi kilichomsibu mtu huyo mpaka kufikwa na mauti ya aina hiyo.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaja jina lake,ameeleza kuwa walipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa kijana mmoja aliYekuwa akichunga ng'ombe katika pori hilo ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja,hali iliyowapekea kwenda moja kwa moja eneo la tukio kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo,lakini kila aliyefika pale hakuweza kumtambua huku wengine wakisema huenda hutu huyo alikuwa ni mgeni kijijini hapo.
Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo ili kuona kama ana taarifa zozote juu ya tukio hilo zinaendelea.
Chanzo>>kigoma24hours blog
1 comment:
Terrible situation..
Post a Comment