Ugonjwa wa mfumo wa mkojo kitaalamu urinary tract infection(UTI) umekuwa
ukisumbua watu wengi. Vimelea vinavyosababisha ugonjwa katika mfumo wa mkojo hukua na kusambaa endapo kinga ya mwili inakuwa ndogo hivyo makundi yaliyo katika hatari ya magonjwa
haya ni watoto chini ya miaka mitano,
wamama wajawazito, wanawake na watu wote wenye upungufu wa kinga.
ukisumbua watu wengi. Vimelea vinavyosababisha ugonjwa katika mfumo wa mkojo hukua na kusambaa endapo kinga ya mwili inakuwa ndogo hivyo makundi yaliyo katika hatari ya magonjwa
haya ni watoto chini ya miaka mitano,
wamama wajawazito, wanawake na watu wote wenye upungufu wa kinga.
Mlezi au mzazi anaweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu kwa watoto kwa kufanya yafuatayo;
1. Hakikisha matumizi sahihi ya dawa za kuzuia bacteria (antibiotics) kwa watoto
kama vile amoxylin na cephalosporin pale
unapoandikiwa na mtaalamu wa
afya.matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizi yanaweza kumuweka mtoto katika hatari zaidi ya kupata maambukizi. pale
unapoandikiwa dawa hizi hakikiksha unampa mtoto kwa wakati husika na dozi sahihi na usizidishe muda wa matumizi bila
ushauri wa daktari.
2. Hakikisha mtoto anakunywa maji mengi kwa siku kulingana na umri wake. mtoto wa miaka 3 na kuendelea anashauriwa kunywa
maji glass 6 mpaka 8 kwa siku ili kuepuka upungufu wa maji mwilini(dehydration)
hali inayomweka katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya mfumo wa mkojo.
3. Njia sahihi ya kumsafisha mtoto wa kike sehemu za siri ni kutoka mbele kwenda nyuma ili kuepuka kusambaza bacteria wa njia ya haja kubwa maarufu kama normal
flora ambao kwa kawaida wakitoka katika njia ya haja kubwa kwenda katika njia ya
mkojo wanasababisha ugonjwa katika mfumo wa mkojo.
Kwa mtoto ambaye ameanza kunawa mwenyewe hakikisha
unamfundisha njia sahihi ya kunawa ili kuepuka maambukizi. Kwa mtoto wa kiume
hakikisha anatahiriwa mapema ili kuepusha hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu na kwa Yule ambaye hajatahiriwa bado
hakikisha unamsafisha ndani ya ngozi ya uume wa mtoto mara kwa mara kuepuka kukua kwa bacteria katika mfumo wa
mkojo.
Na endapo mtoto ameanza kunawa mwenyewe hakikisha unamfundisha njia
sahihi ya unawaji.
4. Epuka matumizi ya sabuni kali zenye kemikali kwa mtoto ambazo zinaweza
kupelekea muwasho unaoweza
kusababisha michubuko katika sehemu za siri hali inayorahisisha maambukizi ya vimelea vya magonjwa ya mfumo wa
mkojo.
5. Hakikisha mtoto havai nguo
zinazombana sana katika maeneo ya siri kwa kumvalisha nguo zinazoruhusu hewa kupita ili kuzuia joto na unyevunyevu
unaoengeneza mazingira mazuri kwa ukuaji wa vimelea vya magonjwa katika mfumo wa mkojo.
6. Hakikisha mtoto anakojoa mara kwa mara na hakai na mkojo kwa muda mrefu.
7. Kama mtoto atakuwa na dalili ya ugonjwa wa mfumo wa mkojo kama vile homa, maumivu wakati wa kukojoa, mkojo wenye mawingu na unaotoa harufu kali
mpeleke mapema katika kituo cha afya nahakikisha unatumia kwa usahihi dawa alizoandikiwa.
Usitumie dawa zozote bila ushauri wa daktari.
No comments:
Post a Comment