Friday, 5 December 2014
ICC YAFUTA KESI DHIDI YA RAIS UHURU WA KENYA
MAHAKAMA ya kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai inayomkabili Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Mwendesha mashitaka Mkuu wa mahakama hiyo, Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta kwa kile alichokisema ni kukosa ushahidi wa kutosha.
Rais Kenyatta alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kutenda uhalifu dhidi ya binadamui wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008.
Baada ya kesi hiyo kusuasua, Mahakama ilimpa Bensouda wiki moja kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya Kenyatta au ifutiliwe mbali.
Katika kesi hiyo, Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu ambapo mwengine katika kesi hiyo ni naibu wake, William Ruto.
Hilo ni pigo kubwa kwa nchi za magharibi ambazo zilipendelea kuona Rais Kenyatta na wengine katika kesi hiyo wanakutwa na hatia na kushitakiwa.
Mara baada ya uamuzi wa mahakama ya ICC kuhusu kufutwa kwa kesi hiyo dhidi ya Uhuru Kenyata, kiongozi huyo aliandika yafuatayo kwenye akaunti yake ya Twitter
"Nimepokea habari kwamba kiongozi wa mashitaka ICC ametupilia mbali kesi dhidi yangu. Daima nimekuwa nikisema kuwa kesi za Kenya ICC ziliharakishwa sana kupelkewa katika mahakama ya ICC bila kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Mara kwa mara nimekuwa nikiwasisitizia wakenya na dunia nzima kuwa sina hatia, uamuzi huu ni afueni kubwa sana kwangu kwani ulipaswa kutolewa miaka sita iliyopita.
Nimefurahishwa sana na habari hizi ambazo nimekuwa nikizisubiria tangu jina langu kuhusishwa na kesi iliyowasilishwa Hague dhidi yangu,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Bahati yake safari hii kuwa huru
Post a Comment