Tuesday 9 December 2014

BILIONEA EMAMI WA NIGERIA AMPATIA TAYO DOLA 350,000/= KAMA BACKUP BAADA YA KUSHINDWA KWENYE SHINDANO LA BBAHOTSHOTS


Mshindi wa pili wa BBAHotshots Tayo Falorin.



Baadaya East Afrika yote kuinua shangwe kubwa siku ya jumapili, Desemba 7 kusherehekea ushindi wa nguvu alioupata Mtanzania Idriss Sultan, kweny BBA hotshots, kulikuwa na stori kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazikuwapendeza watu wengi,kwani ilionekana kama baada ya Nigeria hawakuwa na amani kuukosa ushindi huo na kuona ukija Tanzania.


Bilionea:Ayiri Emami.

Sasa mpya kutoka Nigeria ni kwamba Bilionea mmoja hakupendezwa kuona mwakilishi wao Tayo akitoka Patupu. Bilionea huyo Ayiri Emami amempatia mshiriki wa BBa Nigeria Tayo Folarin pesa ambazo ni zaidi hata ya kiwango kilichotolewa na BBA Hotshots kwa mshindi wa kwanza.

Tunawafahamu mabilionea wachache toka Nigeria, wakiongozwa na Aliko Dangote, Emami leo ameonyesha uwezo wake wa kumpatia Tayo Dola laki tatu na nusu (350,000/=).

Kiasi hicho ni Backup kwa Tayo, ambaye alionekana mnyonge sana usiku  ambao Idriss alitangazwa mshindi.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!