Saturday 6 December 2014

BAADA YA DIAMOND SASA IDRIS

Ndani ya wiki mbili tasnia ya burudani katika Tanzania imepata nafasi ya kujitutumua hivi. Wakati wiki moja imepita tangu msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,
Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz kupata ushindi wa kishindo katika Tuzo za Video za Channel O (CHOAMVA), wiki hii kijiti kinahamia kwa Idris Sultani, Mtanzania ambaye huenda kesho naye akaingia kwenye rekodi iwapo ataibuka msindi barani Afrika katika fainali za Mashindano ya Big Brother Hotshots 2015.

Kwa taaluma Idris ni mpiga picha na msanifu kurasa ambaye alikwenda kushiriki mashindano hayo, alitokea katika Kampuni ya I-View Studios.
Mtanzania huyo yupo kwenye nafasi nzuri ya kuibuka mshindi wa BBA Hotshots 2015 kutokana na kukubalika na Waafrika wengi, akiwa pia mshiriki wa tatu kutoka Tanzania kuingia hatua ya fainali baada ya Mwisho Mwampamba na Richard Dyle Bezuidenhout, aliyekuwa mshindi katika msimu wa pili wa mashindano hayo.
Anawania kitita Dola za Marekani 300,000 sawa na Sh500 milioni, huku akichuana na Butterphly na JJ wote wa Zimbabwe, M’am Bea wa Ghana, Macky2 (Zambia),; Nhlanhla (Afrika Kusini), Sipe (Malawi) na Tayo wa Nigeria.
Fally Ipupa, Bebe Cool kutingisha
Katika fainali hizo, mwanamuziki nyota kutoka Uganda, Bebe Cool anatarajiwa kutumbuiza kwa wimbo wake ‘Love You Everyday’ huku nyota wa muziki, Fally Ipupa akitarajiwa pia kupamba usiku huo wa kihistoria kwa nyimbo zake mbalimbali.
Safari ya Idris BBA
Oktoba 5, Idris Sultan alipoingia katika Jumba la Big Brother, alitangaza rasmi mbele ya mshereheshaji IK kuwa ndani ya jumba hilo amefuata wasichana na siyo kitu kingine.
Hicho ndicho kilichotokea kwani Idris alianza safari yake kwa kumtaka kimapenzi msichana Goitse kutoka nchini Botswana kwa kumwonyesha anamjali na kumwandalia chakula cha usiku akisaidiwa na baadhi ya washiriki wa BBA wakiwamo kutoka Uganda, Kenya na Zimbabwe. Hata hivyo juhudi hizo za mwanzo na karata ya Idris katika BBA, ziligonga mwamba, lakini hakukata tamaa.
Wiki chache baadaye Idris alivunja mlango, baada ya Goitse kumweleza kuwa hamtaki tena. Kosa hilo lilisababisha apewe Idris kupewa adhabu ya kuosha vyombo, kupika na kufanya usafi kwa saa 48.
Adhabu hiyo ilimweka karibu na Samantha kutoka Afrika Kusini, ambaye alikuwa akimsaidia. Goitse alitumia mwanya huo kumuumiza Idris kwa kuchafua vyombo mara kwa mara na kukaa na Arthur, Frankie karibu yake ili kumkera
Urafiki baina yake na Samantha ulishamiri, ndipo Goitse alianza kuingiwa na wivu kwani Arthur na Frankie waliaga mashindano hayo. Hata hivyo, wasichana tofaut ndani ya Jumba la BBA walianza kumhitaji Idris kimapenzi akiwamo Sheillah, aliyekuwa na rafiki wa kiume ndani ya jumba hilo aliyeitwa Nhlanhla.
Wakati hayo yakiendelea, Ellah wa Uganda alikuwa mwiba mkali ndani ya jumba hilo, Idris alikuwa akimshauri, lakini ushauri wake ulimwingiza pabaya baada ya kuvamiwa na Kacey Moore ambaye hakutaka kuingiliwa katika anga zake.
Kacey alimtolea maneno makali Idris akamweleza kuwa ameacha mke na mtoto kwao Ghana na hakufuata mapenzi BBA. Lakini, matokeo yake alijikuta akiingia katika mtego wa Ellah na kutolewa mapema kwenye mashindano. Wiki mbili baadaye, Samantha naye akaaga mashindano hayo na hapo Idris akadondokea mikononi mwa Ellah. Baada ya kupigana kisi zaidi ya mara tatu mrembo huyo, Idris alimweleza kuwa hawawezi kuendelea kwani hahisi kama anampenda.
Ellah alitumia mwanya huo kumwaribia mchezo, matokeo yake Ellah aliaga mashindano Jumapili iliyofuata. Idris alisikitika kwa vimwana wake Ellah na Goitse kutoka kwa mara moja, lakini aliapa kutolia.
Ucheshi, vituko, utani na namna anavyoyachukulia mambo ni baadhi ya vitu vilivyosababisha Idris aanze kuandamwa na washiriki wenzake hasa wa kiume, ili kujaribu kumtingisha katika kiti alichodhani amekikalia peke yake.
Akiwa ndani ya jumba hilo, Idris amewaonyesha watazamaji maisha yake halisi na namna anavyojua kuyachukulia mambo, tofauti na idadi kubwa ya washiriki ndani ya nyumba hiyo. Hilo lilimfanya apendwe si tu na watazamaji, bali washiriki wenzake hasa wa kike ambao walionyesha kumkubali.
Wasifu wake
Idris Sultan ni kijana mwenye umri wa miaka 21, aliyezaliwa na kukulia jijini Arusha. Ni mpiga picha na msanifu kurasa kitaaluma.
Anafurahia kusoma kitabu chochote kilichoandikwa na Dan Brown. Ladha yake ya muziki huipata kutoka kwa wanamuziki mbalimbali akiwamo Chris Brown, Michael Jackson, Usher, Ed Sheeran, Sam Smith, Lana Del Rey na Nina Simone.
Idris anasema kuwa afuati nyayo za mtu mmoja, bali anachukua mazuri yote kutoka kwa mtu yeyote alitefanikiwa, atakayekutana naye. Hata hivyo, anaweka wazi kwamba mama yake ndiye anayemfuata zaidi.
Anasema ameingia Big Brother kwa sababu anataka kuhamasisha watu na kulifanya jina lake liwe kubwa, kwani anaamini Waafrika wa bara nzima la Afrika watakuwa wakimwangalia naye atahakikisha anaonyesha umakini wakw na ubunifu

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!