Tuesday, 2 December 2014

ASANTENI WATANZANIA-DIAMOND


MAMIA ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya jana walijitokeza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumpokea msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ aliyerejea kutoka Afrika Kusini alipotwaa tuzo tatu mwishoni mwa mwiki iliyopita.




Diamond alitwaa tuzo hizo zinazoandaliwa na kituo cha runinga cha Channel O na kuwazidi baadhi ya wasanii nyota wa Afrika.
Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Ntampata Wapi, alipata tuzo ya Msanii bora mwenye kipaji wa Afrika Mashariki, Msanii bora mwenye kipaji anayechipukia na video bora ya wimbo wa Afropop kupitia wimbo wake wa Number One.
Akizungumza uwanjani hapo jana, Diamond alisema ushindi alioupata umetokana na nguvu za Watanzania kumpigia kura. “Sikutegemea kushinda tuzo hizi zote kwa mpigo lakini kwa nguvu za wananchi imewezekana,” alisema Diamond.
“Nawashukuru sana Watanzania, hizi zote ni juhudi zao za kuifanya Tanzania itambulike zaidi kimuziki,” alisema. Aidha, Diamond aliushukuru uongozi wake uliokuwa ukimpa moyo siku zote na kusimamia kazi zake ambayo matunda anayaona. “Sina kikubwa cha kusema zaidi ya kusema asanteni kwa wale wote walionipigia kura,” alisema.
Baada ya kutoka uwanjani hapo, msafara wa Diamond na mashabiki wake ulielekea nyumbani kwake Sinza ukipita barabara ya Nyerere kabla ya kutokea barabara ya Uhuru ambapo shughuli za maeneo hayo na mitaa ya jirani zilisimama kwa muda kupisha msafara na kumshuhudia msanii huyo ambaye karibu muda wote alikuwa amebebwa na mashabiki wake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!