Vyuo vikuu vitatu vya Tanzania ambavyo vilishiriki katika mashindano ya mjadala wa Afrika kuhusu Sheria za kimataifa za haki za kibinaadamu yalioandaliwa na kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC vimeshindwa kufika katika raundi ya mwisho.
Badala yake vyuo hivyo viliondolewa katika raundi za mapema ambapo mataifa manane ya Afrika yalishiriki.
ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa mjini Arusha.
Kulingana na gazeti la the Citizen nchini Tanzania, vyuo vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo kikuu cha Zanzibar.
Katika raundi ya mwisho ya mashindano hayo yaliofanyika mwishoni mwa wiki katika mahakama maalum ya kimataifa inayochunguza mauaji ya kimbari nchini Rwanda ICTR mjini Arusha,chuo cha Strathmore University kutoka Kenya kiliibuka mshindi na kufuatiwa na chuo cha Christian University kutoka Uganda huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka Zimbabwe kikiibuka mshindi wa spika bora.
Raundi ya mwisho ya mjadala huo ilisimamiwa na jaji wa mahakama hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji wa mahakama ya haki katika Afrika mashariki Fanstin Ntezilyayo,John Joseph Wamwara na Mutsa mangezi kutoka ICRC.
Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi kwa washindi aliyapongeza mashindano hayo kama kifaa cha kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya sheria na kwamba itasaidia kuimarisha maono yao katika siku za usoni.
No comments:
Post a Comment