Friday, 28 November 2014

NDOA NDOANO! NIMEMUACHA GADNER- LADY JAYDEE


Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe kuwa ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G Habash imevunjika.
63941_10152405802890025_3495294999548219343_n
























Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner.
Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner lakini alisema alikuwa akiteswa.
Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa siku zote amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi kwenye vyombo vya habari.
“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye media, kwenye magazeti au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote wanachohisi, chochote wanachotaka kusema. Ninavyofikiria mtu anayenipenda mimi alinijua sababu ya muziki na waendelee kuliheshimu hilo, kwasababu kila mtu ana haki ya kuwa na privacy. Ingekuwa kila mmoja angekuwa anatoka kwake anaanza kuelezea mambo yake, mama yake jana walishinda njaa, au mume wake alimfanya hivi, sidhani kama kuna mtu yeyote anapenda kuelezea maisha yake, hata matatizo yake mbele za watu.”
“Kwahiyo mpenzi wako Gadner bado mko naye,” aliuliza mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho na mchekeshaji, MC Pilipili. “Swali nafikiri hujalijibu, umemtosa, hujamtosa?,” aliuliza Fadhil Haule, mtangazaji mwingine wa show hiyo.
“Nimemuacha,” alijibu Jide. “Huyu (Gadner) tumeshamalizana.”


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!