Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu matumizi ya takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.Baadhi ya wadau mbalimbali na wataalam wa takwimu waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam.Mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu mchango wa matumizi ya takwimu sahihi katika maendeleo ya taifa lolote wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.Msanii Stara Thomas (kulia) akiwa na waimbaji wenzake akiwasilisha ujumbe wa matumizi ya takwimu sahihi kupitia wimbo maalum wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyowashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi chini.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza jambo kuhusu athari, madhara na ya matumizi ya takwimu zisizo sahihi.Waziri wa Ferdha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee (wa nne kutoka kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment